....nani hajiheshimu?
Mambo vipi?
Uchaguzi umepita....maisha yameanza upya Jana na Pound imeshuka thamani. Maana Ijumaa ilishuti mpaka kufikia 2,900Tsh(why am i telling you this? Never mind).
Kuna wakati mtu unachoka kujielezea na kuelewesha baadhi ya watu kuwa Mavazi ya mtu sio tabia na mavazi mafupi sio kielelezo cha mtu kutokujiheshimu.
Natambua kuna tofauti ya ufupi wa mavazi kulingana na umri japokuwa umri sio sababu ya mtu kubadilisha style yake ambayo anadhani kuwa inampendeza kulingana na shape yake au kulingana na kuonyesha kilicho "perfect" ili kuondoa attention kwenye kile akionacho kuwa ni "imperfect" (miguu vs sura) hiihihihihi mie.
Sasa unapomuita mvaa nguo fupi kuwa ni Malaya, hajiheshimu au Changudoa(uchangudoa ni kazi japo siiungi mkono) na kumtukuza mvaa mavazi marefu na ya kujificha(eti heshima) lakini ana watoto 3+ kutoka wanaume watatu tofauti unakuwa bwegelao(bongwa la mabwege).
Kabla hujachukia au kuponda vazi la mtu ambalo unadhani kuwa si la heshima....jaribu kuangalia kinachosababisha mhusika kuvaa anavyo vyaa. Pia kumbuka mwili ni wake na anauvika atakavyo kutegemeana na anavyojisikia.
Kama ilivyo kwa wazaa ovyo(wake kwa waume).....kuna sababu ya wao kutoheshimu miili yao (zaidi ni Saikolojia ila wengi ni kutojiheshimu)na kujiachia bila kinga. Wanaume wengi wazaa ovyo wanajisifia "mie dume la mbegu" na wanawake hu-justify kuwa "nimeubwa kuzaa".
Basi hata wavaa nguo fupi wanasababu zao na moja nimeitaja hapo awali.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments