Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mavazi

Msafi au Unajipenda?

Kuwa msafi ni tofauti na kujipenda.....Habari gani? Mimi sio Msaaaaafi to the point nahitaji "Tiba" ya Ushauri Nasaa, lakini napenda kusafisha Bafuni/Chooni na Jikoni (nachukia kuosha vyombo though). Maeneo au vyumba hivyo ni muhimu sana kwangu na kwa familia yangu kwasababu  natumia muda mwingi zaidi. Unapoenda Kushundi sharti utulie kwenye mazingira Masafi, haependezi kushundi(kutoa haja kubwa) huku unahofia kupata Maambukizo. Pengine unaharakisha kutoka na kukatisha Haja yako kwasababu ya harufu ya uchafu mwingine zaidi ya Kinyesi chako. Nahitaji kweli kuelezea kuhusu usafi wa Jikoni au Mahali unapoandalia chakula? Kuna siku nilikabidhiwa Jiko...si unajua wale akina Wifi/Shemeji ukienda kuwatembelea wanataka wakutumikishe? Basi nikapewa Jiko....mwenye Jiko mwenyee anajipenda huyo! Jikoni kwake sasa.....kulikuwa na uchafu worth of 3yrs akyanani nikashindwa kupika ikabidi nisafishe jiko na maeneo ya karibu. Kwenye Sinki kulikuwa na vyombo vichafu worth of 5days(Uanaum

Mvaa Vimini na mzaa ovyo....

....nani hajiheshimu? Mambo vipi? Uchaguzi umepita....maisha yameanza upya Jana na Pound imeshuka thamani. Maana Ijumaa ilishuti mpaka kufikia 2,900Tsh(why am i telling you this? Never mind). Kuna wakati mtu unachoka kujielezea na kuelewesha baadhi ya watu kuwa Mavazi ya mtu sio tabia na mavazi mafupi sio kielelezo cha mtu kutokujiheshimu. Natambua kuna tofauti ya ufupi wa mavazi kulingana na umri japokuwa umri sio sababu ya mtu kubadilisha style yake ambayo anadhani kuwa inampendeza kulingana na shape yake au kulingana na kuonyesha kilicho "perfect" ili kuondoa attention kwenye kile akionacho kuwa ni "imperfect" (miguu vs sura) hiihihihihi mie. Sasa unapomuita mvaa nguo fupi kuwa ni Malaya, hajiheshimu au Changudoa(uchangudoa ni kazi japo siiungi mkono) na kumtukuza mvaa mavazi marefu na ya kujificha(eti heshima) lakini ana watoto 3+ kutoka wanaume watatu tofauti unakuwa bwegelao(bongwa la mabwege). Kabla hujachukia au kuponda vazi la mtu ambalo unadhan