Skip to main content

Posts

Showing posts from November 8, 2015

Mzazi kukupenda zaidi ya wenzio...

Habari ya sasa! Kwa kawaida Mtoto wa Kwanza na yule wa Mwisho kwenye Familia nyingi hutokea kupendwa zaidi na wazazi au Mzazi......wakati mwingine wadogo/wakubwa zake. Sababu ya kuwa "favourite" angalau kwa muda hapa ipo wazi. Mtoto wa kwanza ndio kifungua Familia na huwa peke yake kwa muda mrefu au ikitokea kuna mdogo wake kaja fasta basi ile "huruma" huwafanya Wazazi waongeze attention kwa yule wa kwanza. Mtoto wa mwisho ni mdogo kuliko wote hivyo Wazazi na dada/kaka huwa over protected. Pamoja ya kupendelewa au kupendwa zaidi bado Wazazi wengi huwa hawaonyeshi hilo kwa uwazi ili kuepusha ugomvi au kuwafanya watoto wengine kujiona hawapendwi kwa kiwango sawa. Lakini mnapofikia umri mkubwa unaweza kuona kabisa kuwa Baba na Mama wanampendelea fulani zaidi na hivyo kuanza kujenga chuki au ushindani dhidi ya mwenzenu ambae mnahisi kuwa anapendelewa. Hali hufikia pabaya, mpaka anaependelewa kuanza kujidai na kutumia kupendwa zaidi na Waza