Skip to main content

Mzazi kukupenda zaidi ya wenzio...


Habari ya sasa!

Kwa kawaida Mtoto wa Kwanza na yule wa Mwisho kwenye Familia nyingi hutokea kupendwa zaidi na wazazi au Mzazi......wakati mwingine wadogo/wakubwa zake. Sababu ya kuwa "favourite" angalau kwa muda hapa ipo wazi.



Mtoto wa kwanza ndio kifungua Familia na huwa peke yake kwa muda mrefu au ikitokea kuna mdogo wake kaja fasta basi ile "huruma" huwafanya Wazazi waongeze attention kwa yule wa kwanza. Mtoto wa mwisho ni mdogo kuliko wote hivyo Wazazi na dada/kaka huwa over protected.


Pamoja ya kupendelewa au kupendwa zaidi bado Wazazi wengi huwa hawaonyeshi hilo kwa uwazi ili kuepusha ugomvi au kuwafanya watoto wengine kujiona hawapendwi kwa kiwango sawa. Lakini mnapofikia umri mkubwa unaweza kuona kabisa kuwa Baba na Mama wanampendelea fulani zaidi na hivyo kuanza kujenga chuki au ushindani dhidi ya mwenzenu ambae mnahisi kuwa anapendelewa.



Hali hufikia pabaya, mpaka anaependelewa kuanza kujidai na kutumia kupendwa zaidi na Wazazi wake kama Silaha ya kuwaumiza wenzake hasa kwenye Masuala ya Mali ya Familia. Utakuta yeye ndio wa Kwanza kupewa Kiwanja/Nyumba, yeye ndio anaijua Bank Account ya Akiba ya Siri ya Wazazi wenu, Yeye ndio Mshikilia Hati za Assets zote Ghali za Familia n.k.



Wale ambao wanadhani hawapendwi sawa na mwenzao(mdogo/mkubwa) hujenga Genge dhidi yako bila wewe na Wazazi wako kujua. Unakuwa huna sauti kwenye maamuzi ya Kifamilia......kwamba mchango wako hautwi maanani(unadharauliwa).



Kama Wazazi  bado wapo Hai huwa ni rahisi kuendelea na "undugu" lakini mara tu baada ya Wazazi kutangulia basi wewe uliekuwa Favourite unakuwa umeenda na wazazi wako(ndani ya mioyo yao) japo bado una ishi.


Kwenye Familia yangu baadhi hudhani kuwa Mimi ni Favourite(sababu nilikuja Ulaya hihihihi) ukweli ni kuwa hakuna anaependelewa/aliependelewa, kama yupo basi haikuwekwa wazi na Wazazi wetu. Natambua kuwa Mimi nilikuwa Dad's Girl kwasababu ni Binti wa kwanza, sio mtoto wa kwanza.




Nilipata "presha" ya kujifunza mengi kuliko Kaka yangu ambae ndio mtoto wa kwanza. Pamoja na hilo bado sidhani kama Kaka yangu alikuwa "favourite" ya wazazi wetu kwasababu alikuwa wa kwanza kwenye kila Kitu, Kusoma Shule ya Private(miaka ya 90 kwenda Private ilikuwa Deal), kupata the best School Bag na Saa kutoka Ulaya na pia alikuwa wa kwanza Kupelewa Nje ya Nchi.




Nadhani Baba yangu alikuwa Feminist ( Ndio wanaume pia can be Feminist ujue) kimtindo....kwasababu alinisukuma kuchukua Sayansi(ambayo sikuichukua), Alinisukuma kwenye kujitegemea na msemo wake maarufu "ukimtegemea mwanaume utakuwa Mtumwa maisha yako yote", alinifunza Kunyoosha Nguo (am good at kunyoosha Suruali na Mashari) pia alinifunza Kupika Ugali(alitaka Mimi nimpikie Ugali) nikiwa as young as 8yr old.




Well, my point is mie sio Favourite Child, nadhani Wazazi(hasa baba) kama Baba wengine kwa watoto wao wa Kike, hakutaka nisumbuke ukubwani. Aliniandaa. Nampenda sana tu Baba yangu lakini sio Rafiki yangu, Rafiki yangu ni Mama yangu....haya yametoka wapi lakini sasa?




Nikija kwa Wanangu, Asali wa Moyo anasema nampendelea Binti zaidi kuliko Babuu(hii huwa inaniuma) kwasababu najua kuwa nawapenda wanangu the same but different. Nawapenda individually but mara nyingi namtetea Binti kwasababu ni Mdogo sio kwasababu ni my Fav.....Babuu ni Mbabe/Controling hihihihi typical Kaka mkubwa!


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuchagua Blog hii.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao