Skip to main content

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo.


Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani.


Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake).


Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao Wasenge wenyewe. Kwa huku nimesoma nao, nimefanya nao kazi na kuishi nao(sio nyumba Moja).....



.....wait,Stori Time:  wakati nipo "Foronda" actually nilisoma na mmoja akiitwa "Faruku" kwa Utani....alikuwa akivaa Kaptura fupii na za kubana, pia anafungua vifungo 3 vya juu vya Shati lake hehehehe  wakati Wenzake wakivaa Pensi(zinafika Magotini na pana kiasi) na Mashati ya kawaida ya Shule. Daily alikuwa akichapwa kwa kutovaa Sare sahihi mpaka wakamzoea!



Sasa wapo walioamua kuendele kuwa "Wasenge" kwasababu ya Mazoea, kwamba walikuwa-abused kwa muda mrefu walipokuwa wadogo.  Vilevile kuna wale wanaamua kugeuka/kugeuza ili kujikimu(lifestyle), Wengine hutokea tu (naturally) kuwa wanavutiwa na Jinsia kama zao..iwe kuingiliwa au kuingilia au vyote.



Nisiwasahau wale ambao hujikuta wanapenda kuwa kama Wanawake/Wanaume au wanaamini kuwa wao ni Wanawake/Wanaume ila wameumbwa na maumbile yasio sahihi na mwisho kabisa tunao wale Wanaume wanaopenda kujiremba na kuvaa kama Wanawake.


Msenge sio Lazima avae na kuongea kama Mwanamke au kujiremba, hata Mumeo na Misuli yake anaevaa Kiume anaweza kuwa Msenge pia. Kumbuka Usenge kwa Wanaume sio Kuingiliwa tu bali hata kumuingilia Mwanaume mwenzio ni Usenge....nyie mnaita Basha!! Pia Wasenge wengi hawana Gender roles kwenye mahusiano yao.



Kwahiyo sasa Msenge au Wasenge hawawaibii Wanaume/Wapenzi wenu, bali Wanaume wenu ni Wasenge to begin with.....hali na uwezo wa kusimamisha mbele ya Mwanaume Mwenzio, kuingia, kufanya na kumaliza....huo ni Usenge 100% ila unajificha kwenye Ubasha kibongo-bongo. Basha ni Msenge, Mumeo sio Basha wala Bisexual...Mumeo/Mpenzi wako ni Msenge full stop!! Usijipe moyo...ooh tumezaa, ooh anasimamisha daily. Nani alikuambia Wasenge hawasimamishi?



Wasenge wa Mjini hawaibi Wanaume, isipokuwa ninyi Wanawake hamjui kuwa  Wanaume wenu ni Wasenge.....kumbuka Wasenge wanawajua Wasenge wenzao ambao bado hawajitambua(wamejificha kwenye kivli cha Ubasha) au wanajitambua ila kutokana na aibu wanaamua kufunga ndoa na kuwa na familia kama Jamii inavyotaka. Lakini huko nje huitwa maBasha ambapo wengi hudhani kuwa ni "sifa" na inakupa "muonekano" wa kuwa Mwanaume wa "kweli" na pengine kuogopwa Mtaani kwasababu unainamisha/pindisha Wanaume wenzio. Lakini kihalisia wao ni Wasenge/mashoga pia.



Ushoga Tanzania haujaanza leo, nani anamakumbuka Shoga Maarufu aitwae Farook ambae alikuwa mcheza Ngoma Asilia maarufu pale Zanzibar(nilisimuliwa na Marehemu Bibi)....Mtu kuwa Ushoga/Usenge sio  Kosa Kisheria, isipokuwa kufanya Mapenzi kinyume na Jinsia (kulawiti) ndio Kosa, sasa iwe unaingiliwa na Mumeo huko Tigoni au Mwanaume anaingilia wanaume wenzie ni Kosa kisheria.



Kutokujua kunakufanya kuwa Muoga, kuhofiwa kuibiwa Bwana/Mume.....ukijifunza kuhusu hii Jamii utaelewa na hakika hautokuwa Muoga na kamwe hautojenga Chuki dhidi ya hawa watu. Utawachukulia kama walivyo na maisha yataendelea kwa amani kabisa.


Nathamini muda wako hapa na ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "