Skip to main content

Posts

Showing posts with the label magufuli

Kama Mumeo anakupenda hatoruhusu ufanye haya...

Kutokana na wakati tuliopo ambapo  kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi  ukweli kuwa kuwa Mwanamke  mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada. Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true  kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa  kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa. Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni n...

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak...

Jinsi ya kukabiliana na Mwanaume apendae kununa/susa/chuna...

Sio kwamba anapenda (hakuna mtu anapenda kununa)isipokuwa anatabia ya kununa(Kislani/Gubu). Kama ilivyo kwa sisi Wanawake , wenzetu pia huwa wananua ila kununa huko huwa wanakupa Jina lingine tofauti kabisa na Kisilani/Gubu ili wasihusishwe na "Uanamke"(wakiamini ni udhaifu na Mwanadamu pekee dhaifu Akilini mwao ni Sisi). Utamsikia anang'aka na kusema hana gubu/hajanuna/hajajitenga isipokuwa "siku yangu imeharibika/imeanza vibaya", "usinisumbue nina Mawazo", "Nahitaji muda wa peke yangu kutuliza akili", "Najisikia vibaya" na ikiwa alipoteza Mzazi au Wazazi wote basi hiyo itatumika zaidi..."nimewakumbuka Wazee" nakadhalika. Tabia hiyo inakera na inaumiza sana, inakupa wewe Mke mtu upweke wa hali ya juu. Inaweza kukupa ushawishi kwa ku-check na Ex au hata kutamani kutafuta kipoozeo. Hivyo kusababisha mtikisiko kwenye Ndoa/Uhusiano wenu ikiwa hakuna Mawasiliano au hamjuani(hamjasomana tabia, kwamba bado ni Wapenzi wap...

Rudisha Heshima ya Ndoa: Jinsi ya kuepuka Ulalamishi/Kosoaji too Much.

Kama wewe ni Mkosoaji, hii inakuhusu zaidi, Karibu. Ndoa kama Ndoa ni ngumu na inahitaji  kufanyiwa kazi kila Siku kutoka pande zote mbili. Ndoa  ni ya wawili sio jukumu la Mke tu au Mume tu, bali  nyote kwa pamoja. -Angalia yaliyo Chanya zaidi ya Hasi. -Kubali kuwa Makosa yako kimaisha kabla yake(Mwenza wako) hayamuhusu....kwamba kutotimiza Ndoto zako ni Makosa yako wewe na yeye hausiki. Kwa pamoja  manaweza  kukamilisha Ndoto mpya kama Mke na Mume kwa Ushirikiano na Support bila Kumlazimisha afanye yale utakayo wewe kufidia uliyofeli kabla hajakutana. -Tambua kuwa unaweza kuwa unamjua Mkeo/Mumeo vema sana baada ya kumsoma lakini bado huwezi kamwe kusoma Akili yake. Epuka kusema "najua unachofikiria" "najua unachokitafuta", "najua kwanini unafanya hivyo" n.k....jifunze kutumia maneno "wakati mwingine unanifanya nadhani blah blah blah"...if anything. -Kubali kuwa wewe haujakamilika, kwasababu mwenza wako hakukosoi au halalamiki haina m...

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...

...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani? Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme. Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme  kama uliikosa. Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe. -Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona...

Akisema "tafuta mwingine, mie siwezi/nimechoka"....

...hamaanishi kwamba ukatafute  kweli mwingine, anachomaanisha ni kuwa "nibembeleze na unihakikishie kuwa utanivumilia" mpaka nitakapo kaa sawa Kihomono au kupona(kama alikuwa anaumwa)....Za Miezi Miwili/Mitatu? hello, jambo jambo!! Kwa kawaida Mume anapopatwa na tatizo kubwa litakalomfanya ashindwe kutekeleza Majukumu yake kama Baba na Mume, Mwanamke atavumilia na kumuuguza, kumpa Moyo na Matumaini. Lakini Mwanamke akijifungua(zaa) achilia mbali kuugua....katoa Uhai wa Mtu salama baada ya Miezi 9 kukaa na kulala kwa tabu. Mara zote kipindi hiki huwa Kigumu sana japokuwa kasumba ya Jamii "kukuharakisha" upone haraka huficha ukweli kuwa Mwanamke anapojifungua hukabiliana na mambo mengi Kiafya(kimwili, kihisia na kiakili). Hali ambayo hufanya baadhi ya Wanaume kuamini kuwa Mimba na kuzaa ni "cha mtoto" tu, sio kazi(kama alivyo pizi ndani ya dakika zake 3 kwa utambu uliodumu kwa sekunde 90)....hakuna ugumu wowote, fyatueni tu. Kwa kawaida(uzoefu wa...

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mumeo ajihisi "Mfalme"....

Waliposema "ajihisi Mfalme" hawakumanisha akutawale na kukutumikisha wewe Mkewe kama Mtumwa wake na hivyo kukosa sauti na kubaki "Ndio bwana", bali kufurahia maisha ya Ndoa na hivyo kurudisha ufanyao ili na wewe ujihisi "Malkia"......Heri ya Mwaka mpya 2017!! Mie kama Mwanandoa wa "Kitambo" sasa nimeamua Mwaka huu kurudisha Heshima ya Ndoa baada ya kuona kuwa watu wanapotosha na  hivyo Ndoa kuonekana kuwa ni Kazi...well ni Kazi ya pili baada ya ile uifanyayo kukupatia Kipato au ya Tatu ikiwa mna watoto, lakini sio Kazi kwamba ni ngumu na ukibaki humo basi wewe ni Shujaa. Hapana! Upotoshaji huo unapelekea baadhi ya watu waliokwisha "onja" Ndoa na baadae kuharibika kuchekwa/shangawa kwanini wanarudi tena Ndoani(na watu mwingine) wakati tayari wanajua "maumivu" ya Ndoa....Vijana wamekuwa wakiiogopa Ndoa. Kwasababu Ndoa moja imeharibika haina maana zote zitakuwa kama hiyo iliyopita. kumbuka watu wanatofautiana na pia kuna...

How to kaza K baada ya Usiku...

...wa Tendo tayari kwa "cha" Asubuhi. Niligusia kuwa baadhi yetu(mie) huwa hatuogi baada ya Tendo Usiku, tunalala nayo ili kuachia "nature" ifanye yake(itoke yenyewe) pia  ili kutunza Utamu si eti! Maana ukikimbilia kuoga unasahau hata kama ulipata! Inategemea na Imani yako, pia inategemea unaichukuliaje Manii. Mie Binafsi Manii sio Uchafu ikiwa mwenye nayo ni Mume wangu. Ikiwa ni Mpita Njia kwamba hamna uhusiano ambao ni  "exclusive na serious" hakika Manii ni Uchafu na kamwe Usikubali yabaki Ukeni which means post hii haikuhusu hihihihi  natania usiondoke mwaya! Sijui kama unajua ila Ukikaa na Manii K-ini unakuwa hatarini kuwa "over relaxed" huko chini hivyo ikifika Asubuhi  hutofurahia Tendo kiviiiiiiiiile! Hata wakati wa kusaka Mimba hunashausiwa kukaa nayo kwa Dakika 5-15 ukiwa umejinua ili kuharakisha prosesi. Pia ukikaribia kujifungua unashauriwa kucha Manii humo muda mrefu uwezavyo ili kukusaidia wakati wa kujifungua...kwamba ...

Mwenza Mshindani/Mpinzani...utamjuaje?

Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote. Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa  Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam). Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo  kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe...

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"...

...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini? Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa  ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo. Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake. Wapo ambao hu...

Nini Mbadala wa kuomba radhi kwa Mwenza?

Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha. Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu? Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa  Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume). Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na...

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet...

....sio kiviile ila close(I promise)....Jello! Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello? Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao? Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya.  Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba. Sasa pamoja na ...

Kukabiliana na Mwenza/Mpenzi "mpya" baada ya Miaka kadhaa...

....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa . Upo salama lakini?....twenzetu! Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko. Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu). Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone...

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao...

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......

....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini? Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu. Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Ha...