Skip to main content

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"...



...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini?



Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo.



Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake.


Wapo ambao husema Nakupenda mara kadhaa kwa siku, pia wapo ambao wanasema hivyo wakati wa kufanya Mapenzi tu na wachache husema hivyo siku wakiwa na Furaha au Hatia (wamefanya kosa) etc....sio unafurahia"I love you" kizembe zembe....wengine wanakuwa wametoka kiunoni kwa mwingine na wanakupigia Simu na kukuambia wanakupenda....shauri yako!



Leo hapa tukumbushane namna nyingine ambayo Mwenza wako anakuambia anakupenda bila kutamka hilo neno. Inategemea na Wenza husika, namna nitakazokutajia ni za Kiujumla ambazoo wengi wanaweza kuzifanya....mwenza wako anaweza kufanya zaidi kulingana na Uhusiano wenu na jinsi mnavyojuana.


1-Jinsi anavyokufanya, na huwa anafanya Mapenzi zaidi ya Ngono...unajua tofauti si eti?(Mwanaume).

2-Jinsi anavyokuangalia(wote)...hujawahi kaa  mahali na kumuangalia Mumeo/Mkeo na kujisema "hata siamini Miaka yote hii naneng'enuka na huyu Kaka na bado ni Moto"?

3-Namna anakupa "nafasi" mnapokuwa kwenye manunuzi....mf: Halipi mpaka ahakikishe umefurahia na kuridhika(Mwanaume).

4-Anawahi Nyumbani kabla yako na kufanya kila kitu(Mwanamke)

5-Anakuheshimu...Mf: Haleti  Marafiki/Ndugu Nyumbani bila kuhakikisha kama utakuwa okay na Ugeni(Wote).

6-Anakutambulisha kama Mke/Mume na sio Mama/Baba Mama/Watoto(wote).

7-Anakuwa na "kawivu" na anakuambia kuwa alishikwa na Wivu. mf. amekuona kwa mbaali mahali alipokuwa "mapumziko" na akakupigia Simu nakukuambia amekuona sehemu fulani na akirudi nyumbani hali inakuwa si hali...yaani mapenzi Moto Moto(sio kupigana).

8-Wewe ni Rafiki yake, Mshauri wake na mara nyingi anakuambia wazi kabisa kuwa hana Rafiki kama wewe.(Wote)


Ongezea yako basi eti...Post Ijayo tuangalie yule Mwenza  anaekupenda sana lakini anakuchukulia wewe kama "Mpinzani" badala ya "partner"...Usikose!


Ahsante kwa kuichagua Blog hii, kama kawaida  naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.

Babai.

Comments

.. said…
Ndoa yangu ilikuwa karibu kufikia mwisho nilipoona maoni juu ya mtu anayeitwa Dr DAWN ambaye husaidia watu kuwarudisha wenzi wao na niliwasiliana naye kwa bahati nzuri kwangu aliniroga baada ya masaa 24 mpenzi wangu alirudi kwangu tangu wakati huo ndoa yangu imekuwa. amekuwa mtulivu asante kwa yote aliyonifanyia naweza kukuhakikishia kuwasiliana naye,
yeye ni mjuzi wa maneno yafuatayo:
* maneno ya mapenzi
*miujiza ya ndoa
* uchawi wa pesa
* bahati nzuri
* Vivutio vya ngono inaelezea
* UKIMWI Tiba Uchawi
* Pango la Casino
* Mapango Yamelaaniwa Yameondolewa
* Ulinzi Spell
* Uchawi wa bahati nasibu
* Maneno ya Bahati
* Tahajia ya Uzazi
* Pete ya Telekinesis
WhatsApp: +2349046229159

Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao