Skip to main content

Posts

Showing posts with the label msamaha

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"...

...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini? Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa  ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo. Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake. Wapo ambao hu...

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo? Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo. Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k. Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke! Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi...