Skip to main content

Posts

Showing posts from September 6, 2015

Penzi la Kwanza halikufi(halifi)....

Well Penzi lolote la Kweli halifi/halifagi na penzi hili huwa halitokei kila mara, ikitokea limetokea(hilo Penzi la kweli) basi mtu unakuwa umefika.....kama ni Safari ya Reli ya Kati basi Umemaliza...upo Kibondo Kigomaaa. Pamoja na kufika kwako Kibondo( Kimapenzi) bado huwezi kusahau yule uliempenda Kweli(au kwa mara ya kwanza....sio Ngono kwa mara ya kwanza, wacha haraka). Sasa hii ni mchanganyiko wa penzi hilo "kutokufa" au wewe kukumbuka hisia ulizozipata baada ya kuwa na huyo Mwanamke/Mwanaume ambae hana uhusiano na wewe Kidamu (sio Mama/Baba).....sote tunajua namna ya kupenda na kupendwa Wazazi wetu sio? Mwanaume wa kwanza kumpenda ni Baba yako(ikiwa wewe ni Mkimama) na Mwanamke wa kwanza kumpenda ni Mama yako(ikiwa wewe ni Mkibaba). Hisia za kumpenda mtu baki ni nzuri na wakati mwingine zinachanganya(kuujua Ujinsia wako).....unaeza kujikuta unashindwa kutambua ni yupi hasa unampenda kiukweli(hisia hizi ni Mpya na ni tofauti na za kumpenda Babako).....ukako

Marafiki(best) ni Milele, Wapenzi waja na kuondoka....

....kweli kabisa (kama upo chini ya miaka 29). Unapofikia umri mkubwa mambo mengi yanabadilika na unajikuta kuwa huitaji Marafiki ili kuwa na furaha(kufurahia Maisha yako). Sio hivyo tu pia unakua/badilika(nao pia) na hivyo mnakuwa hamuendani tena kama ilivyokuwa enzi zile, Matokeo yake unakuwa unafahamiana na watu na sio kurafikiana nao(best friends eeh Siwezi!). Marafiki wanakusaidia kujifunza kuhusu Maisha (kihisia), wanakusaidia kujua namna ya kukabiliana na Drama za "maisha", wanakusaidia kujua  nini cha kudharau/kushikilia Bango, wanakusaidia kujua kuwa wewe upo tofauti nao, wanakusaidia kujuana nini cha kuchangia/kutokuchangia, wanakusaidia kujua ni wakati gani unatakiwa kuachana na jambo na kusonga mbele, wanakusaidia kuelewa jambo/somo Darasani (tunauelewa tofauti) n.k. Hivyo ni Muhimu sana tena sana kwa Mtoto kutengeneza Marafiki ili aweze kujifunza hayo niliyoyataja hapo juu. Sio kila kitu Mtoto anajifunza kutoka kwa Wazazi, mengine anajifunza akiwa S

Kujiamini kwa Mtoto kunaanza lini?

....Watoto wa "Ulaya" wanajiamini sana, je kuna namna ya kulea mtoto ili akikua ajiamini kama wa Ulaya? Mkaka mmoja aliniuliza. Nadhani wengi wetu tumeaminishwa Mengi ya Ughaibuni ni Mazuri/Mema....lakini katika hali halisi sivyo. Kuna soko zuri sana la Vitabu/Vipindi vya TV vinavyofunza Wazazi namna ya kulea watoto wenye Kujiamini. Ni tatizo la Wazazi husika ambao walilelewa "Kimaendeleo" na hivyo kuhofia kuwa watoto wao watakuwa kama wao. Hofu hiyo inawafanya wazazi kuwa-overprotect watoto. Nahisi tu sina uhakika. Kujiamini kunategemea zaidi na Malezi(nakubali) lakini sehemu kuwa ya Mtu/Mtoto kujiamini inatokana na yeye mwenyewe alivyoumbwa. Niliwahi kugusia Bloguni hapa kuwa kuna baadhi tumezaliwa hivyo(tunajiamini) lakini pia wapo ambao hawajiamini mpaka wafunzwe/himizwa/pewa Moyo/saidiwa kujiamini. Naamini Watoto wa Afrika(well Tanzania wa kizazi kileeee) tunajiamini kwasababu tulitumia muda mwingi kujifunza kimwili na sio kihisia kama watoto