Skip to main content

Penzi la Kwanza halikufi(halifi)....

Well Penzi lolote la Kweli halifi/halifagi na penzi hili huwa halitokei kila mara, ikitokea limetokea(hilo Penzi la kweli) basi mtu unakuwa umefika.....kama ni Safari ya Reli ya Kati basi Umemaliza...upo Kibondo Kigomaaa. Pamoja na kufika kwako Kibondo( Kimapenzi) bado huwezi kusahau yule uliempenda Kweli(au kwa mara ya kwanza....sio Ngono kwa mara ya kwanza, wacha haraka).





Sasa hii ni mchanganyiko wa penzi hilo "kutokufa" au wewe kukumbuka hisia ulizozipata baada ya kuwa na huyo Mwanamke/Mwanaume ambae hana uhusiano na wewe Kidamu (sio Mama/Baba).....sote tunajua namna ya kupenda na kupendwa Wazazi wetu sio? Mwanaume wa kwanza kumpenda ni Baba yako(ikiwa wewe ni Mkimama) na Mwanamke wa kwanza kumpenda ni Mama yako(ikiwa wewe ni Mkibaba).





Hisia za kumpenda mtu baki ni nzuri na wakati mwingine zinachanganya(kuujua Ujinsia wako).....unaeza kujikuta unashindwa kutambua ni yupi hasa unampenda kiukweli(hisia hizi ni Mpya na ni tofauti na za kumpenda Babako).....ukakosa usingizi na kuanza kuwaza. Majamaa watano wanakufukuzia(nazungumzia mabinti  kwa uzoefu hapa)! Wote wanatofautiana Kimuonekano, Kimtazamo,Kiutongozaji,Kiuchumi(wazazi wao obviously)....aah unaona ya nini nawatolea wote Nje....bado mdogo mie.





Muda unafika unahisi sasa upo tayari kwa "mapambano" lakini tatizo wafuatiliaji wote wamesonga Mbele na hawana mpango na wewe, hata salamu hawakupi.....kama unabahati basi hawatokuwa wamekuzushia kuwa "aah yule Demu yule, hamna kitu, nilshamtia mara kibao" hihihihi the Low life type of  Wavulana.




Inakuja tokea tu umekutana na Mjamaa na Kemikali ikakubali, anakuheshimu, anakupenda,anakujali, hana haraka na kuneng'enuka, anakununulia zawadi, anakusaidia homework, anakufuata shuleni au anakusubiri Kituoni kwako ili tu apate Muda wa kuongea na wewe. Rahaaaa! Miaka inapita, huna uhakika kama ni Mshkaji(nyie mnaita Boyfriend)  au ni Rafiki? anyway tukatishe hadithi.....mnakuwa Wapenzi kwa mara ya kwanza. Baada ya miaka kadhaa mnajikuta mnataka vitu tofauti Maishani.....labda mmoja anataka Ndoa na Familia, Mwingine anataka Kusoma zaidi. Manaachana.





Huyo Mtu (penzi la kwanza) atabaki Moyoni kwa Muda mrefu na pengine kukufanya ushindwe kuwa na Mpenzi mwingine, si kwasababu unataka au kuombea/tarajia kuwa nae tena huko mbeleni la Hasha! ni kwamba huoni kama ni fair kuwa na mtu mwingine wakati Moyo upo kwingine(am single and happy ndio huja hapa au Shule/Kazi ndio Mpenzi wangu).




Miaka inapita, anatoka Moyoni na sasa unakuwa wazi na huru  kuruhusu mtu mwingine akae Moyoni mwako(zaidi ya Yesu, bwana apewe Sifa hihihihi), inaweza umelamba Dume au ikawa Galasha/sa hisia sio kama zile za "Penzi la kwanza" unajiengua kwake....by the time unalamba Dume  na ushakuwa Mtu mzima na unarejea tena Kibondo tena kwa Mara ya Pili, lakini hii safari ya sasa inaondoa kumbukumbu za ile ya kwanza, mazingira ya Kibondo sio yale tena, Migahawa/Maduka na Wamiliki ni tofauti, unajua Mitaa zaidi ya ile iliyo karibu na Stesheni.....nakupoteza eti? kwa kifupi Penzi hili linafunika/Zika lile la Mwanzo.





Unagundua kuwa Penzi hili ni tofauti kabisa  na lile la "kwanza" na hapa unagundua kuwa uzoefu ulioupata mwanzo ulikuwa mwanzo wa safari yako ya kujifunza kupenda nje ya kumpenda Baba na Mama na hakika hisia zile zilikuwa nzuri kwasababu Mpenzii ana-offer mambo ambayo baba/mama yako hawezi/hapaswi/nikosa kisheria/ni dhambii kukufanyia.





Pamoja na kusema hivyo bado ukimkumbuka/ukikumbuka jinsi mlivyokuwa enzi hizo(sasa ni jitu tofauti na pengine linatisha) unapata tabasamu usoni na kujisemea moyoni "aaah nilimpenda sana yule jamaa". Wakati mwingine inaeza kuwa  "nikukitana nae tena lazma nitamuonyesha how nimekuwa in er bed?"(sikutumi ukafanye hivyo, nasema tu kufurahisha Genge la Wahuni).




Hizi ni hisia ambazo sote huwa  nazo, lakini sio sahihi kudikilea kwa kila mtu kuwa "Daima nitampenda yeye "......unawajua wale "mama/baba wa wanangu, daima nitampenda".....no dear daima utamheshimu(wakati umem-cheat kwa  mfano).....huwezi kumpenda mtu wakati hutaki kuwa nae kama Mkeo/Mumeo. Duuuuh! nimehamia kwingine, ngoja nikaji-fix-ie a Cuppa!


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao