Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mapenzi

Mambo 7 Mumeo angependa umfanyie, ila...

...anaogopa kukuambia. Heri ya Mwaka mpya 2023 kwanza, leo google wamenitumia "data" bana, wanasema mwezi wa january kumekuwa na watu Laki nane na Eflu 11(8.11K) wametembelea Blog hii....nikasema Mayooo wane nimezeeka! nilikuwa napata idadi hiyo kwa Siku😅anyways, kama wewe ni mmoja wao basi nasema ahsante sana. Naendeleaje bila twita kwa Miezi 7? Vema kabisa, ahsante kwa kujali. nimegundua kuwa nina Muda mwingi sana wa kufanya mambo mengine muhimu kwa ajili ya afya ya Akili yangu. Ila baada ya kugusa miezi 4 hali ilianza kuwa ngumu nikawa nawakumbuka wote ambao tulikuwa tunabadilishana twiti mara kwa mara nikataka kushusha App, nikapata nguvu za kughaili, nikashida.  Vipi Mumeo na wanenu 3? Bado tumeshikiliana kwa mapenzi ya dhati, wanetu wanaendelea vema pia shukurani. Sema nini gharama na uhitaji wa kugawa "attention" kwa individual's umri na mahitaji yao Kiakili, Elimu, Malezi na "daily Activities" yameongezeka hyuuu!! Ila kwenye mambo mengine wan

Nguzo 5 za Mahusiano bora(Masikilizano/Maelewano).

Masikilizano/elewano huja wakati/baada ya mawasiliano japo ni Nguzo inayoweza kusimama peke yake kutegemea na tukio....mf:- wakati wa manunuzi makubwa(gari, nyumba), familia yenu iwe na watu wangapi?, Shule/Malezi ya watoto na pengine “career”. Unapowakilisha jambo/kero kwa mwenza wako ni vema kuwa katika hali ya utulivu(sio mara zote hufanya kazi hasa kama mwenzio sio msikilizaji mzuri). Utulivu wako husaidia kutoongea kwa sauti ya kushambulia na hivyo kuepeuka yeye kujitetea(bila shambulio hakuna pa kurudisha shambulio). Unapoibua suala ili lizungumzwe/jadiliwe nia ni kufikisha Ujumbe/kero na kupata muafaka(maelewano) na sio kung'aka na kuanza kugombana....hii hupoteza muda(kusumbua watoto kihisia/akili) na tatizo kuzimishwa badala ya kumalizwa. Kuzima/acha tatizo bila muafaka/maelwano kwa muda mrefu hupelekea mwanzilishi wa “mazungumzo" kuhisi kuwa hasikilizwi na hisia zake hazithaminiwi na mwenza wake. Hisia hizo hupelekea hasira(jitahidi kujizuia ili usifanye jambo mbaya)

Nguzo 5 za Mahusoano/Ndoa Bora...

Nguzo 5 za Mahusiano bora ya Kimapenzi ilikuwa topic maarufu sana 2007. Unakumbuka? Nilizielezea kwa kirefu kama utambulisho, wakati ule wengi walikuwa hawafahamu na baadhi hawakuwa wameziishi. Sasa tangu umeziishi nineona sio mbaya kama nikizirudia tena kwa pembe tofauti kidogi na ile ya 2007. Kabla sijaenda huko hebu nikukumbushe Nguzo hizo ambazo ni... 1) Mawasiliano. 2) Maelewano/sikilizano 3) Ushirikiano 4) Heshima 5) Kujali Ni rahisi kudhani kuwa wewe na Mwenza wako mnafanya yote hayo na kuamini kuwa Uhusiano wenu upo Imara. Utajuaje kuwa Mawasiliano ni mabovu? Mara ya mwisho kukaa chini na kuzungumza masuala yenu binafsi na yale ya kimaendeleo? Je, mwenzako anapokuja na hoja, huwa unasikiliza, jadili inapobidi na kufikia maelewano?  Ikiwa Mara zote mnaishia kubishana badala ya kujadili sababu mmoja wenu kapandisha sauti(foka) basi ujue uhusiano wenu hauna mawasiliano. Ni muhimu kutafuta namna ya kurekebisha na kuboresha kona hiyo. Njoo tena tuseme kuhusu Masikilizano kwa pembe t

Muendelezo wa Twiti yangu ya "if he is hot, don't let yourself go"...

Miaka mitatu iliyopita niliandika kuhusu Wanaume wapenda nachuro byuti, kama ilikupta isome hapa  kisha tuendelee. Kwanza habari za leo? mie nipo Likizo, aina ya Likizo ambapo unafanya yote uyafanyayo unapokuwa nyumbani isipokuwa haupo nyumbani. Achana na hili. Kuwa shabiki wa "natural beauty" wakati unavaa Nguo, unaoga maji Safi ya Bomba(yana Kemikali), unavuta hewa kila siku(imejaa toxic), unakula vyakula vinavyotunzwa kwa kutumia Kemikali ili kuepusha magonjwa/wadudu, Ukiugua unatumia Tiba ya Kisasa, Unatumia Simu kuwasiliana  n.k. sio rahisi. Hakuna tatizo la mtu kupenda Urembo wa Asili na hakuna tatizo kwa yeyote anaependa Urembo wa kununua/jiongezea ailimradi tu hambadilishi na kukufanya uonekane mtu mwingine. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kusakama Wanawake wanaopenda kujiremba(usually wasio kuwa na pesa, maana makeups sio chee). Kutokana na maisha yalivyo  hivi sasa (Wanawake tunafanya yaliyokuwa yakifanywa na Wanaume pekee) na mabadiliko ya Hali

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak

Jinsi ya kukabiliana na Mwanaume apendae kununa/susa/chuna...

Sio kwamba anapenda (hakuna mtu anapenda kununa)isipokuwa anatabia ya kununa(Kislani/Gubu). Kama ilivyo kwa sisi Wanawake , wenzetu pia huwa wananua ila kununa huko huwa wanakupa Jina lingine tofauti kabisa na Kisilani/Gubu ili wasihusishwe na "Uanamke"(wakiamini ni udhaifu na Mwanadamu pekee dhaifu Akilini mwao ni Sisi). Utamsikia anang'aka na kusema hana gubu/hajanuna/hajajitenga isipokuwa "siku yangu imeharibika/imeanza vibaya", "usinisumbue nina Mawazo", "Nahitaji muda wa peke yangu kutuliza akili", "Najisikia vibaya" na ikiwa alipoteza Mzazi au Wazazi wote basi hiyo itatumika zaidi..."nimewakumbuka Wazee" nakadhalika. Tabia hiyo inakera na inaumiza sana, inakupa wewe Mke mtu upweke wa hali ya juu. Inaweza kukupa ushawishi kwa ku-check na Ex au hata kutamani kutafuta kipoozeo. Hivyo kusababisha mtikisiko kwenye Ndoa/Uhusiano wenu ikiwa hakuna Mawasiliano au hamjuani(hamjasomana tabia, kwamba bado ni Wapenzi wap

Rudisha Heshima ya Ndoa: Jinsi ya kuepuka Ulalamishi/Kosoaji too Much.

Kama wewe ni Mkosoaji, hii inakuhusu zaidi, Karibu. Ndoa kama Ndoa ni ngumu na inahitaji  kufanyiwa kazi kila Siku kutoka pande zote mbili. Ndoa  ni ya wawili sio jukumu la Mke tu au Mume tu, bali  nyote kwa pamoja. -Angalia yaliyo Chanya zaidi ya Hasi. -Kubali kuwa Makosa yako kimaisha kabla yake(Mwenza wako) hayamuhusu....kwamba kutotimiza Ndoto zako ni Makosa yako wewe na yeye hausiki. Kwa pamoja  manaweza  kukamilisha Ndoto mpya kama Mke na Mume kwa Ushirikiano na Support bila Kumlazimisha afanye yale utakayo wewe kufidia uliyofeli kabla hajakutana. -Tambua kuwa unaweza kuwa unamjua Mkeo/Mumeo vema sana baada ya kumsoma lakini bado huwezi kamwe kusoma Akili yake. Epuka kusema "najua unachofikiria" "najua unachokitafuta", "najua kwanini unafanya hivyo" n.k....jifunze kutumia maneno "wakati mwingine unanifanya nadhani blah blah blah"...if anything. -Kubali kuwa wewe haujakamilika, kwasababu mwenza wako hakukosoi au halalamiki haina m

Rudisha Heshima Ya Ndoa: Mwenza hana Jema, kila siku Kukosoa...

Kukosoana ni jambo jema na muhimu ili kusaidia kurekebisha Tabia ndogo-ndogo ambazo ni mbaya lakini kumkosoa  Mwenza wako mara kwa mara (kupitiliza) bila wewe mwenyewe kujali kuwa unakasoro zako ambazo anazivumilia ni wazi utakuwa Mnyanyasaji. Unyanyasaji huo utamfanya mwenzio kujisikia vibaya na hivyo kusababisha:- -Maumivu ya Hisia na Akili. -Kumfanya Mwenzio ajione hana thamani au Umuhimu kwenye Ndoa yenu. -Uoga/Hofu  kwenye Ndoa yenu -Kuondoa Furaha na hivyo kujitenga kihisia -Kukosa Amani -Msongo wa Mawazo Kwasababu Mwenza wako sio Mlalamishi au Mkosoaji wa mara kwa mara haina maana kuwa wewe ni Mungu na hukosei, kwamba wewe ni next to perfect(hakuna binadamu asie na Kasoro) ndio maana Mkeo/Mumeo hajawahi kukukosoa au kulalamika. Ukweli ni kuwa, baadhi ya Weza huwa "wanakurekebisha" kwa vitendo, kwamba anafanya exactly vile unapaswa kufanya au kwa kukupa "hints" bila kuumiza Hisia zako wala kusababisha ujisikie vibaya. Asipo pata matokeo ndio ana

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...

...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani? Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme. Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme  kama uliikosa. Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe. -Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa

Akisema "tafuta mwingine, mie siwezi/nimechoka"....

...hamaanishi kwamba ukatafute  kweli mwingine, anachomaanisha ni kuwa "nibembeleze na unihakikishie kuwa utanivumilia" mpaka nitakapo kaa sawa Kihomono au kupona(kama alikuwa anaumwa)....Za Miezi Miwili/Mitatu? hello, jambo jambo!! Kwa kawaida Mume anapopatwa na tatizo kubwa litakalomfanya ashindwe kutekeleza Majukumu yake kama Baba na Mume, Mwanamke atavumilia na kumuuguza, kumpa Moyo na Matumaini. Lakini Mwanamke akijifungua(zaa) achilia mbali kuugua....katoa Uhai wa Mtu salama baada ya Miezi 9 kukaa na kulala kwa tabu. Mara zote kipindi hiki huwa Kigumu sana japokuwa kasumba ya Jamii "kukuharakisha" upone haraka huficha ukweli kuwa Mwanamke anapojifungua hukabiliana na mambo mengi Kiafya(kimwili, kihisia na kiakili). Hali ambayo hufanya baadhi ya Wanaume kuamini kuwa Mimba na kuzaa ni "cha mtoto" tu, sio kazi(kama alivyo pizi ndani ya dakika zake 3 kwa utambu uliodumu kwa sekunde 90)....hakuna ugumu wowote, fyatueni tu. Kwa kawaida(uzoefu wa

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mumeo ajihisi "Mfalme"....

Waliposema "ajihisi Mfalme" hawakumanisha akutawale na kukutumikisha wewe Mkewe kama Mtumwa wake na hivyo kukosa sauti na kubaki "Ndio bwana", bali kufurahia maisha ya Ndoa na hivyo kurudisha ufanyao ili na wewe ujihisi "Malkia"......Heri ya Mwaka mpya 2017!! Mie kama Mwanandoa wa "Kitambo" sasa nimeamua Mwaka huu kurudisha Heshima ya Ndoa baada ya kuona kuwa watu wanapotosha na  hivyo Ndoa kuonekana kuwa ni Kazi...well ni Kazi ya pili baada ya ile uifanyayo kukupatia Kipato au ya Tatu ikiwa mna watoto, lakini sio Kazi kwamba ni ngumu na ukibaki humo basi wewe ni Shujaa. Hapana! Upotoshaji huo unapelekea baadhi ya watu waliokwisha "onja" Ndoa na baadae kuharibika kuchekwa/shangawa kwanini wanarudi tena Ndoani(na watu mwingine) wakati tayari wanajua "maumivu" ya Ndoa....Vijana wamekuwa wakiiogopa Ndoa. Kwasababu Ndoa moja imeharibika haina maana zote zitakuwa kama hiyo iliyopita. kumbuka watu wanatofautiana na pia kuna

How to kaza K baada ya Usiku...

...wa Tendo tayari kwa "cha" Asubuhi. Niligusia kuwa baadhi yetu(mie) huwa hatuogi baada ya Tendo Usiku, tunalala nayo ili kuachia "nature" ifanye yake(itoke yenyewe) pia  ili kutunza Utamu si eti! Maana ukikimbilia kuoga unasahau hata kama ulipata! Inategemea na Imani yako, pia inategemea unaichukuliaje Manii. Mie Binafsi Manii sio Uchafu ikiwa mwenye nayo ni Mume wangu. Ikiwa ni Mpita Njia kwamba hamna uhusiano ambao ni  "exclusive na serious" hakika Manii ni Uchafu na kamwe Usikubali yabaki Ukeni which means post hii haikuhusu hihihihi  natania usiondoke mwaya! Sijui kama unajua ila Ukikaa na Manii K-ini unakuwa hatarini kuwa "over relaxed" huko chini hivyo ikifika Asubuhi  hutofurahia Tendo kiviiiiiiiiile! Hata wakati wa kusaka Mimba hunashausiwa kukaa nayo kwa Dakika 5-15 ukiwa umejinua ili kuharakisha prosesi. Pia ukikaribia kujifungua unashauriwa kucha Manii humo muda mrefu uwezavyo ili kukusaidia wakati wa kujifungua...kwamba

Mwenza Mshindani/Mpinzani...utamjuaje?

Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote. Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa  Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam). Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo  kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe

Nini Mbadala wa kuomba radhi kwa Mwenza?

Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha. Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu? Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa  Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume). Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet...

....sio kiviile ila close(I promise)....Jello! Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello? Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao? Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya.  Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba. Sasa pamoja na

Je ni Muhimu kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mpenzio....

...just incase? Mie binafsi siwapendi Rafiki zake wote...well sio wote, wapo  ninaowapenda ila Asali wa Moyo hayupo karibu nao so nimebaki na nisio wapenda which means siwapendi WOTE!! anyway... Siku nkaenda shiriki Semina ya Wanandoa Wachanga(mie mepita Miaka Saba so nilienda kama Mzoefu). Dunia ya leo watu wanadanganyana sana aisee. Mke wa Pastor aliedumu kwenye Ndoa kwa Miaka 28, akawa anashauri Wanawake walio Ndoani ambao hawana "uzoefu". Mengi yalisemwa ila lililonigusa ni hili la LAZIMA na MUHIMU sana kuwa karibu na Rafiki wa Mumeo, just incase siku moja mkikorofishana na wewe ukashindwa kuongea moja kwa moja na Mumeo. Kwamba unaenda kwa Rafiki yake/zake na kuwaomba wamfikishie ujumbe....au "Ongea na mwenzio, maana mimi hanielewi" Kweli Mama Pasta? kweli kabisaa?? Huyu ni Mume wangu(najisema kimyomoyo Seminani), tulipokula Kiapo ilikuwa kati yake Yeye, Mimi na Mungu  na tuna-share kila kitu(isipokuwa Miswaki na DNA?) ikiwa kuna issue kati yetu Mam

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo? Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo. Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k. Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke! Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi

Je ni lazima atiki viboksi vyako vyote vya Mr wright?

Mwaka ukianza ila mtu hujitahidi kujiwekea List ya mambo/vitu ambavyo angependa kuvifanya au kufanikisha Mwaka husika. Mimi Binafsi kinachobadilika huwa  ni Namba tu na hivyo Mipango yangu huwa haitegemei Mwanzo wa Mwaka. Naweza kuanza Machi nikafanikisha June au nisifanye lolote la ziada kwa mwaka mzima. Furahia maisha huku ukipiga hatua taratibu bila kujiwekea "dead line"(ndio naamini). Pamoja na kusema hivyo bado siwezi kukataa kuwa sote huwa tuna "aina" ya mtu ambae tungependa kubarikiwa enough na hivyo kuwa  nae na kuchangia yale Mazuri, Mabaya na ya Ovyo maishani na hata kuanzisha Familia pamoja. Tena ukiwa katika umri mdogo (miaka 21-30)hali huwa mbaya ziadi.....unatolea  nje watu kibao kwasababu sio "type" yako. Yaani kwnye viboksi 10 anatick 2 tu! Sikuzaliwa tu nikawa 30+ nilipitia unayopitia wewe, na hakika list yangu ya Mr right ilikuwa ndefu kuliko yako.....na hiyo ndio sababu sina List ya Exes kwasababu nilitaka yeyote atakae "

Mzunguuko wa Ngono kwa Mwanamke...

Jambo! Kama unakumbuka niliahidi kuwa nikipata muda nitaandika kuhusu Mzunguuko wa Hedhi ambao unaendana na Mzunguuko wa Kufanya Ngono/Mapenzi kwa Mwanamke. Nilielezea kuwa Mwanamke sio kama Mwanaume, kwamba tunakabiliana na mambo mengi ukiachilia mbali Homono(Pengine ni Homono tu). Kuna siku Mwanamke analianzisha, inaweza kuwa mara moja au tatu kwa mwezi. Pia kuna siku mwanamke anataka kuwa Juu sio kwasababu wewe Mkibaba unataka bali mwili wake unamtuma kutaka kuwa in-control na hii inaweza kutokea mara kadhaa ndani ya mwezi lakini sio kila siku. Hali kadhalika zipo siku(ambazo ni nyingi) mwanamke anataka kuhisi kupendwa  na kujaaliwa kwa vitendo(kitandani)......vinginevyo Tendo halitokuwa na maana na halitokuwa la kufurahia. Wale Wanawake na Wanaume mabingwa wa kuwalaumu wanawake kuwa ndio sababu ya Waume zao kutereza nje ni ama hawaujui Mwili wa Mwanamke, kwamba mwanaume ataka na kutegemea Mwanamke awe in control kila siku......au kungojea Mwanamke alianzishe ili afurahi

Umuhimu wa Furaha ya Mke....

....wengi huchukulia suala hili juu juu tu, labda hushindwa kuelewa kwasababu Jamii (ikiongozwa na wanawake wenyewe) huwa  hailizungumzii sana kama wazungumziavyo Furaha ya Mume. Furaha ni hitaji la wote lakini nadhani kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwasababu bila furaha kwake ni wazi watoto  na baba mtu hatokuwa na furaha. Pia furaha kwa mwanamke inahusika sana kwenye masuala ya kufanya mapenzi.....kama mwanamke hana furaha ni ama hakutakuwa na Tendo au Tendo halitokuwa la kufurahia na badala yake litakuwa ni la kumaliza haja tu kwa Mwanaume(maliza nilale arrg hihihihi). Wanaume wachache ambao wameshuhudia baba zao wakihakikisha Mama zao wanafuraha mara zote iwezekenavyo, hujitahidi na kuwa hivyo au zaidi kwa wake zao. Hawa hujua namna ya kujali  na kuheshimu hisia za mwanamke. Kwabahati mbaya sehemu kubwa ya Wanaume wamelelewa kwenye Mazingira ya kumuona Mama  ni mtu mmoja mvumilivu, mpole na muelevu.....wakati Baba Mkali na Bingwa wa kudharau. Kwamba Mama anapochoshwa n