Kukosoana ni jambo jema na muhimu ili kusaidia kurekebisha Tabia ndogo-ndogo ambazo ni mbaya lakini kumkosoa Mwenza wako mara kwa mara (kupitiliza) bila wewe mwenyewe kujali kuwa unakasoro zako ambazo anazivumilia ni wazi utakuwa Mnyanyasaji. Unyanyasaji huo utamfanya mwenzio kujisikia vibaya na hivyo kusababisha:-
-Maumivu ya Hisia na Akili.
-Kumfanya Mwenzio ajione hana thamani au Umuhimu kwenye Ndoa yenu.
-Uoga/Hofu kwenye Ndoa yenu
-Kuondoa Furaha na hivyo kujitenga kihisia
-Kukosa Amani
-Msongo wa Mawazo
Kwasababu Mwenza wako sio Mlalamishi au Mkosoaji wa mara kwa mara haina maana kuwa wewe ni Mungu na hukosei, kwamba wewe ni next to perfect(hakuna binadamu asie na Kasoro) ndio maana Mkeo/Mumeo hajawahi kukukosoa au kulalamika.
Ukweli ni kuwa, baadhi ya Weza huwa "wanakurekebisha" kwa vitendo, kwamba anafanya exactly vile unapaswa kufanya au kwa kukupa "hints" bila kuumiza Hisia zako wala kusababisha ujisikie vibaya. Asipo pata matokeo ndio anaweza kukuambia.
Ni vigumu sana kuishi na Mwenza wa hivyo kutokana na maumivu anayokupa. Sasa kabla hujaanza kupanga namna ya kuikimbia Ndoa yako, tulia kwanza nikuambie nini cha kufanya, Jinsi ya kuepuka....ila kabla tuanze na sababu zinazoweza kupelekea Mwenza kukukosoa kupita Kiasi(kuku nyanyasa Kihisia/Kiakili).
Nini hasa huwa kinasababisha Mkosoaji kupitiliza?
-Hawana raha/furaha na jinsi walivyo na hivyo wanataka na wewe uwe kama wao bila kujua.
-Majuto; inawezekana kutokana na Makosa yao ya Maisha huko nyuma kabla yako.
-Fainali Uzeeni, hajafanikiwa kukamilisha Ndoto zake na hivyo anatupia "Mpira wa lawama" kwako kama sababu ya yeye kufeli/kutofanikiwa(Wakati hukuwepo wakati wa Ujana wake).
-Malezi/Makuzi mabovu aliyopitia....ama hakulelewa na Wazazi moja kwa moja bali Ndugu kama vile Dada/Kaka/Bibi/Babu n.k. kwa zamu, kwamba hakuwa na "Stable family" utotoni mpaka utu Uzima.
Nini cha kufanya:-
-Usiwe Hasi kwake wala kumkosoa(rudishia). Mwache atiririke na wewe Msikilize kwa makini ili upate materials/points za kutumia Moto wake ukipoa. Usisababishe Mabishano hasa kama mna Watoto.
-Utakuwa umeumia sana kihisia(kwa kawaida kama Mwanamke utakuwa umemchunia), pamoja na maumivu hayo jitahidi kufikiria yote anayokukosoa/lalamikia kila siku. je yanajirudia? je kuna mabadiliko umefanya(jirekebisha)? je haoni jema pamoja na kuwa umejirekebisha? je alikuwa amekunywa kidogo?( ona point ifuatayo hapo chini)
-Baada ya Maumivu/Mnuno/Chunio kuisha, Mwambie ungependa mzungumze. Utakapo anza kuzungumza nae mwambie wazi kuwa ungependa mzungumze na sio mbishane, kwamba akusikilize.
-Ongea nae kwa Upole lakini kwa kumaanisha tena kwa kumuangalia Usoni moja kwa moja. Mwambie tabia yake ya kulalama/kosoa kila akipata nafasi inavyokufana ujisikie. Weka wazi kuwa huna furaha tena kwenye Ndoa yenu kutokana na Tabia yake hiyo mbaya(nafasi yako kumkosoa hii, itumie vizuri. Simamia kwenye yeye kukukosoa kupita kiasi na alivyokufanya ujisikie, mengine save ili usimuumize).
-Mwambie ni sawa kukukosoa lakini sio sahihi kurudia yaleyale kila mara bila kuangalia kama umefanya mabadiliko, pia sio vema kila mnapokuwa pamoja yeye ni kukosoa tu. Mwambie hudhani kuwa hakuna jema hata Dogo ufanyalo na kustahili kukusifia/shukuriwa. Mpe mfano wa Mema unayodhani unafanya kwenye Ndoa yenu au kwenye Malezi ya Watoto wenu.
-Malizia kwa kusema, nisingependa Ndoa yetu iishie pabaya na nisingependa watoto wetu wawe wanakusikia ukilalamika kila siku kwa mambo yale yale au pengine kusingizia ili upate nafasi ya kukosoa.
Una nyongeza? swali je? tupia humu dinahicious@gmail.com
Sijibu Email moja kwa moja bali nitaweka hapa kwa faida ya wengine.
Nathamini na kujali Muda wako hapa, ahsante.
ooh Post ijayo itakuwa Jisni ya Kuepuka Ukosoaji wa Mara kwa mara, Usikose
Bai
Comments