Skip to main content

Posts

Showing posts from July 13, 2014

Nipo mtaani kwako, upo home?...

Sipendi hii tabia kwa Moyo Mkunjufu kabisa!!! Nilikuwa namkimbia rafiki yangu Mghana kwa tabia hii....niambie basi siku moja kabla hujaja kuwa unapanga kuja kwangu....sio unafika Mtaani kwangu au pengine Mlangoni halafu ndio unaniambia kwa Simu! Sio peke yake, hata ndugu (wa mbali) na jamaa wanatabia hiyo....kuna siku (nikiwa bado Nyumbani) nilimrudisha mtu kwao on next flight....the next Bus bana, hela ya next flight mie ninayo?!!....nikaambiwa nina Roho Mbaya. Katoka huko Mwanza sijui wapi eti kaja kutafuta Kazi, asa kwanini usituambie mapema tujiandae na Bajeti!....anyway achana na hilo. Mie huwa sifanyi jambo ambalo najua sipendi kufanyiwa, tatizo linakuja pale Mwenza wako sasa anatabia hiyo....hehehehe Baba Babuu Asali wa Moyo wangu bana anaudhi kweli!!! Mnaweza mkawa safarini mara akakumbuka fulani anakaa karibu na hapo mnapopumzika labda....ananyanyua simu "eh bwana fulani! Upo nyumbani?....tupo hapa karibu kama vipi tuje kuwasa

Make up artists....

Ukiingia kwenye Department stores au Boots (Duka la Dawa na Vipodozi) kubwa kwa sie wa Ulaya hii hapa....unakutana na MUA kwenye "viOSK" vyao wenyewe wamejiremba wamependeza....er kwa mbali! Asa sinilikuambia tangu nigonge miaka 30....sasa ni 30na nimeanza "kuipenda" ngozi yangu ya usoni! "Mambo ya mwanamke reception".....sasa kama mtu hukujaaliwa "reception" nzuri au kurembeka(mimi) basi angalau Ngozi iwe nzuri na yenye afya kuwapotezea watu "focus". Mwanamke nimejaribu bidhaa kibawoo za kufanya Uso wangu uwe laini na wenye rangi moja....maana...mmh! Sijawahi kutumia Mkorogo (na sina mpango huo), sina tatizo na Chunusi (mpaka nile Chocolate), yaani ngozi yangu inakaribia ukawaida tu japo inatoa mafuta ya kutosha kukaangia Vitumbua....anyway! Nimejaribu skin care nilizokuwa nikitumia miaka ya nyuma in my late 20s, sasa zinadunda, kitu cha uso ama kimekomaa au kimekuwa Sungu (Kisayansi ngozi hupoteza n

Kabla hujafa, hujaumbika!

Ni kawaida ya watu (wengi) kucheka matatizo ya wenzao au kuyazungumzia katika mtindo wa "kichekesho". Mimi napenda sana kucheka na kuchekesha (japo kuwa sichekeshi....yaani nikitoa kichekesho watu hawacheki mpaka nielezee kwanini nilichosema kinachekesha)....hihihihi achana na hili! Matatizo nayogusia hapa ni yale ambayo mtu hana uwezo wa kuyazuia, sio matatizo ya kujitakia(kuchagua) kama vile Utumiaji wa Madawa (japokuwa hata hawa mie huwa siwacheki). Kama huna utu na huna mpango wa kumsaidia mwenye matatizo kwanini uzungumzie matatizo yake kwa watu wengine katika hali ya "kumcheka"? Wengine wanapoleta habari za mtu za kusikitisha kutokana na matatizo yake yaliyobadilisha Mwili au Akili (Ulemavu) yake hawacheki kwa kukenua Meno, lakini jinsi wanavyoelezea unagundua kabisa wanamcheka mhusika. Mf; "Eh bwana unamkumbuka Elia? Daah jamaa yaani kaisha halafu sasa anatembelea Mgongo. Yule jamaa alikuwa anajifanya mjanja sana"....umeona? Hakenui meno laki