Skip to main content

Kabla hujafa, hujaumbika!

Ni kawaida ya watu (wengi) kucheka matatizo ya wenzao au kuyazungumzia katika mtindo wa "kichekesho". Mimi napenda sana kucheka na kuchekesha (japo kuwa sichekeshi....yaani nikitoa kichekesho watu hawacheki mpaka nielezee kwanini nilichosema kinachekesha)....hihihihi achana na hili!


Matatizo nayogusia hapa ni yale ambayo mtu hana uwezo wa kuyazuia, sio matatizo ya kujitakia(kuchagua) kama vile Utumiaji wa Madawa (japokuwa hata hawa mie huwa siwacheki). Kama huna utu na huna mpango wa kumsaidia mwenye matatizo kwanini uzungumzie matatizo yake kwa watu wengine katika hali ya "kumcheka"?


Wengine wanapoleta habari za mtu za kusikitisha kutokana na matatizo yake yaliyobadilisha Mwili au Akili (Ulemavu) yake hawacheki kwa kukenua Meno, lakini jinsi wanavyoelezea unagundua kabisa wanamcheka mhusika.



Mf; "Eh bwana unamkumbuka Elia? Daah jamaa yaani kaisha halafu sasa anatembelea Mgongo. Yule jamaa alikuwa anajifanya mjanja sana"....umeona? Hakenui meno lakini maelezo yake yanaonyesha kumcheka Elia.


Usicheke Matatizo ya mwenzio ungali bado unaishi na Muombe Mungu wako unaemuamini (maana wapo Wengi siku hizi) aendelee kukulinda na siku yako ya kufa ikifika ufe hivyo hivyo kama alivyokuumba (ulivyozaliwa)....Maini, Ubongo, Ngozi, Kongosho na mengineyo yarudi kama yalivyokuwa.....THEN ukiwa Ahera wacheke wote walio na matatizo yaliyowabadilisha Miili au Akili.


Babai
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao