Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kiswahili Tanzania

Kabla hujafa, hujaumbika!

Ni kawaida ya watu (wengi) kucheka matatizo ya wenzao au kuyazungumzia katika mtindo wa "kichekesho". Mimi napenda sana kucheka na kuchekesha (japo kuwa sichekeshi....yaani nikitoa kichekesho watu hawacheki mpaka nielezee kwanini nilichosema kinachekesha)....hihihihi achana na hili! Matatizo nayogusia hapa ni yale ambayo mtu hana uwezo wa kuyazuia, sio matatizo ya kujitakia(kuchagua) kama vile Utumiaji wa Madawa (japokuwa hata hawa mie huwa siwacheki). Kama huna utu na huna mpango wa kumsaidia mwenye matatizo kwanini uzungumzie matatizo yake kwa watu wengine katika hali ya "kumcheka"? Wengine wanapoleta habari za mtu za kusikitisha kutokana na matatizo yake yaliyobadilisha Mwili au Akili (Ulemavu) yake hawacheki kwa kukenua Meno, lakini jinsi wanavyoelezea unagundua kabisa wanamcheka mhusika. Mf; "Eh bwana unamkumbuka Elia? Daah jamaa yaani kaisha halafu sasa anatembelea Mgongo. Yule jamaa alikuwa anajifanya mjanja sana"....umeona? Hakenui meno laki