Skip to main content

Posts

Showing posts from March 22, 2015

Ile Manukato ya Kiume uitakayo...

Mambo? Miaka ya nyuma nilikuwa nina aina mbili tu za Manukato.....moja ya Jioni (Organza) na nyingine ya kutwa nzima(Eden) harufu zake zinadumu muda mrefu....huitaji kujimwagia tena. Nikaja kukutana na mdada mmoja anapenda Manukato kupita kiasi....kwamba akiwa na pesa ya ziada lazima anunue.....tena Designer ones. Nikawa namshangaa nikisema anahitaji signature kwa maana aina moja au mbili tu za harufu basi nikawa namuita perfume addict. Sasa leo hii napanga makorokocho yangu jikagundua nina Chupa kama Nane hivi za Manukato.....ama kweli hujafa hujaumbika! Kati ya hizo zote my classicO Organza haipo sababu iliniudhi nilipokuwa mjamzito kwa mara ya kwanza.....will have to revisit(kuinunua tena).....ila Eden made it! Unajua pale unapendezwa na Manukato ya Kiume sio harufu yake tu bali Chupa husika inapendeza ukiiweka pale kwenye dresser si eti? Basi unajifanya umemnunulia Asali wa Moyo kumbe kiukweli umejinunulia mwenyewe kwasababu huwezi kujipulizia Manukato ya kiume basi unamnusa

Best Umri wa kufurahia Maisha.

Habari yako? Je kuna umri uliopita na ukadhani ulifaidi sana na kufurahia maisha kuliko sasa au miaka michache kati kabla ya umri ulionao sasa? Sijawahi kufanyiwa au kufanya sherehe ya siku ya Kuzaliwa sio tu kwa sababu za Kikacha kuwa hatuna hizi mambo (unaiga tu) lakini pia binafsi sipendi mikusanyiko ya watu na ikiwa naeza kuepuka kwa kutokuwa na Party basi na iwe hivyo....so yeah. Naishi kwenye Nchi ambayo kutimiza miaka fulani ni big deal na hivyo mhusika kutaka ku-share siku yake maalum na watu wengine. Hiyo ni Kacha yao na hivyo inawafanya (Kazini wanajua DoB na anuani yako so huna jinsi)baadhi wanipatie zawadi na hapo ndio suala la "am too old for the party ila zawadi napokea" linakuja  badala ya kuzikataa. Kuna umri ambao nahisi nilifurahia zaidi maisha yangu na hivyo kuzipenda namba au umri huo uliopita. Sikuwa chini ya Wazazi na sikuwa na majukumu. Nilifanya maamuzi bila kujali watu wengine....Baada ya hapo nikawa busy  na maisha. Tangu Kibibi(princess) ameac

Mwanao anapoleta the Ex Factor

Kwa wale ambao Uhusiano wa bf na gf uliharibika na kuvunjika kwa sababu zozote na kwa bahati mbaya mlizaa (ukizaa na mtu halafu ni X mwenzangu ni bahati mbaya). Sasa imagine kila unapowakorofisha watoto......watoto hukasirika tu hata kwa yale mema kwao.....mf unawakataza wasicheze Jikoni ni hatari au unahimiza wafanye home work badala ya kutazama Tv. Kila unapokwenda kinyume na watakavyo kama mzazi kwa faida yao wanaanza kulia au kununa na kumtaja mama au baba yao......"Baba angekuwepo ingekuwa hivi au vile" au "mama angekuwepo asingenikataza hili au lile" na hiyo huwaongezea huzuni na hata kilia kwa Uchungu bila wewe kuwaona. Mara chache unaweza kusikia wakimtaja mzazi mwenzio ambae ni mama au baba yao lakini umeachana nae na sasa unamchukia. Nimesema hayo yote kutokana na tabia ya Babuu pale unapomuudhi(ukimkataza kufanya kitu).....ananuna halafu anasema "I want my dad to come and cheer me up". Maneno hayo hunifanya nimuonee huruma (ndio atak