Skip to main content

Posts

Showing posts from June 22, 2014

Kaja for a reason....

Wacha kujipa Moyo.....hakuna mtu anajiijia tu maishani mwako isipokuwa wewe unaruhusu awe/aingie Maishani mwako. Ukisema umefanya maamuzi mabaya ya kuruhusu huyo particular mtu maishani mwako nitakuelewa. Kumbuka wewe ndio responsible kwa kila kinachotokea maishani mwako iwe ni maamuzi mazuri au mabaya.....beba mzigo na ujipange upya, sio kujipa-jipa moyo...eti sababu Mzungu anakuaminisha kuwa "people come in your life for a reason". Kuna watu wanaishi ili kuharibu maisha ya watu, ndio furaha yao. Wengine walikosa mapenzi na malezi bora kutoka kwa Wazazi/Walezi matokeo yake wanayatafuta waliyoyakosa kwa kuharibu maisha ya wenzao.....nakadhalika. Sasa ni juu yako kumsoma yeyote anaekuja maishani mwako na kumruhusu aingine kama Rafiki, Mpenzi, Jamaa ( wale mliooa/olewa Ukoo Mmoja), ukigundua tu kuwa umekosea basi haraka muepuke kabla hajaharibu zaidi. Nikupe mfano?....I looooooooooove mifano hihihihihi(watu tunauelewa tofauti, bila mifano wengine tunatoka kapa). Unaishi maisha

Mali ya Familia...

Kuna baadhi yetu tunatabia/kasumba ya kuita Mali za watu kuwa zetu na pengine kuanzisha fujo na kupelekea Vita kubwa ili kila mmoja apate "mgao" wake. Kwasababu tu Mali ni za Baba/Mama yako au Kaka/Dada yako haikupi haki ya wewe kupata Mgao....wacha papara za kutaka kunijibu, nitakupa mfano ili unielewe vema. Baba na Mama wameachana wakiwa hawana kitu, Baba kaanzisha uhusiano mwingine na kupata familia "mpya"....mambo yakaenda vema wakawa na Mali za kutosha....wewe uliezaliwa na Mama wa kwanza unadhani una unahaki na Mgao sawa kama watoto waliomo kwenye "familia Mpya"? Upatikanaji wa Mali za Baba yako na familia yake Mpya unamchango Mkubwa wa Mama yao (familia Mpya) na sio Mama yako (alieachana na Baba yako akiwa hana kitu)....sehemu ya mali utakayoipata ni ndogo sana, tena kama Mke atakubali upatiwe. Mf; wa kwanza. Mf wa Pili: Dada/Kaka kajipinda na kujituma yeye na Mume/Mkewe na sasa wanamiliki Mali nzito, inakuaje wakubwa/wadogo watu mhesabu kuwa hizo

Weusi mzuri...

If you have to tell us then it isn't....Mambo vipi? Weusi wa Afrika tuna issues zetu ambazo zinasababishwa na Watawala wetu(Siasa)....ila Weusi wa Wamarekani wana issues vichwani mwao kuhusu Weusi wao, yaani wapo ka' Mikorosho vile. Ujue kunatofauti ya kujivunia ulivyo na kulazimisha watu wajue kuwa unajivunia ulivyo. Mf: Kuna ulazima gani wa kusema "mimi ni mweusi na ninajivunia" wakati tunakuona wewe ni mweusi, unajipenda, unapendeza na unafanya mambo yako kama watu wengine. Kwanini utulazimishe kutambua kuwa "unajivunia"? Mf wa pili; Kitu gani kinakufanya uweke "kichwa cha habari" cha video/picha na kusema "beautiful black baby"....kwani ukiandika "baby" au "beautiful baby" haileti maana au hakuna watoto weusi na wazuri isipokuwa huyo wako? Unatulazimisha kutambua kuwa unajivunia Weusi wako alright, lakini picha/video "unazipausha" ili zionekane na karan