Tuesday, 28 December 2021

Kujali(nguzo 5 za Mahusiano.

 Huwezi kuwa Mke bora ikiwa hufanyi mambo Milioni moja na nusu ikiwa ni pamoja na Kujali. 


Kujali kwenye Ndoa  sio kitu kinachotakiwa kufanywa na Mke, bali Mume pia. Japokuwa  kwenye jamii Mke ndio hutegemewa kuonyesha kujali zaidi kuliko mwenza wake wa kiume.Mke atahakikisha Mume analala mahali safi na comfortable, nyumba safi na inapendeza, Nguo na hata Chakula kimeandaliwa vema na kwa wakati.Mke hatoishia hapo, atajiswafi na kujiremba/pendezesha/nukia vizuri kwa ajili ya Macho na Heshima kwa Mume(watu watakao kuona nje).


Mke ataendelea kutoa ushari, kumtuliza, kumpa moyo/matumaini, kum-support, kuhakikisha ana Afya njema na kumkumbusha suala zima la kuilinda Afya yake.Ikiwa mnaishi mbali na Wazazi wa Mume, Mke atakumbusha kuwajulia hali na pengine kwenda kama Familia ili wasipoteze ukaribu kwako na Wajukuu zao.Mwisho kabisa, Mke atahakikisha watoto wanakubuka siku Muhimu kwa Baba yao na kukupatia vijizawadi kwa niaba yao(Watoto)
 


Uliza Mumeo anakujali kwa 
kufanya nini? Kwa 99% atasema “naenda Kazini kila siku ili kulinda na kulisha familia yangu”.


Hutofurahia hilo jibu kwasababu huko sio kukujali bali kutimiza Wajibu wake kama Mume....maana na wewe(pengine Dada wa Kazi) unalinda, tunza, lea, fundisha watoto wenu.


Unajua kwanini Mumeo hajali kama unavyojali wewe?

Ni kwasababu  Mwanaume haandaliwi  kuwa Mume bali Mhudumia familia iwe Wazazi wake ama wadogo zake, ntugu na jamaa.


Ili mumeo aonyeshe kukujali inabidi uwe wazi na kumwambia ni nini hasa unataka akufanyie nini?

Monday, 29 November 2021

Nguzo 5 za Mahusiano...Heshima kwa Mumeo.

Nilikuacha solemba eti, natumai upo salama,..mie mzima kabisa ahsante kwa kujali.
Bila shaka unewahi kuona/soma/sikia watu wakisema "Mwanaume haitaji kupendwa bali kuheshiniwa", kwamba Heshima kwake ndio kupendwa...lies the Internet tells.Mwanaume anahitaji vyote, Heshima na kupendwa....ila ukifikiria kiundani(inategemea na situation iliyokufanya ushushe heshima kwake ) kumpenda Mume wako bila kumheshimu ni ngumu. Acha kufikiria kiundani.
Pengine Mumeo amewahi kukuambia kuwa anahisi kuwa huna heshima kwake...halafu ukang'aka na kudai sio kweli, kwamba mbona unamheshimu sana tu!
Heshima kwa Mwanaume(Mumeo) ni tofauti na vile unamuacha anajiachia kwenye Internet/Bar na wadada wengine, kutopinga maamuzi yake hata kama ni mabaya/hatarishi, kutokuvaa mavazi fulani n.k.Hivi ndio unavyopaswa kumheshimu Mumeo ukiachilia mbali kumsikiliza pia usizungumzie mapungufu yake kwa watu wengine hata kama ni Mama yako.Thamini Ndoa yenu (sio kuishi kwa mazoea) na ikitoke mmepishana na kugongana/zozana chunga Ulimi wako na usitumie Lugha/maneno ya kudhalilisha.Ikitokea amekushirikisha kwenye jambo la familia na akakupa nafasi ya kufanya uamuzi....onyesha kumuamini yeye kufanya uamuzi huo kisha subiri majibu, sio kurudi na kuanza kumbugudhi na maswali.
Badala ya kwenda kwenye Social media/kwa Rafikizo/Wazazi kuomba Ushauri, omba ushauri kwa Mumeo. Pengine Mumeo sio mshauri mzuri kwenye baadhi ya mambo(inategemea na Upeo/Elimu/Uzoefu) bado mmpe hiyo heshima.Akiamua kusaidia kwenye suala fulani hapo nyumbani muamini na muache afanye mpaka mwisho....unless otherwise atakuomba msaada, usiingilie au kukosoa akifanyacho.


Ni kawaida kwa Mumeo kukataa adharani kuwa ahitaji kusifiwa, kupewa attention au kuhakikishiwa Penzi ulilo nalo kwao. Ukweli ni kwamba hawa viumbe wanahitaji kusifiwa kama vile sisi tunavyopenda tofauti wqo hawahitaji mara nyingi kama sisi.Sifia mumeo akitokelezea(pendeza), akikamilisha jambo(kubwa au dogo),  mhakikishie kuwa unampenda na hakuna mtu atachukua nafasi yake(kwa vitendo pia)Je unajiheshimu na unamheshimu Mkeo ili akuheshimu au nikukumbushe pia?


Muda wako hapa ni thamani kubwa kwangu, ahsante.

Wednesday, 25 August 2021

Nguzo 5 za Mahusiano bora(Masikilizano/Maelewano).

Masikilizano/elewano huja wakati/baada ya mawasiliano japo ni Nguzo inayoweza kusimama peke yake kutegemea na tukio....mf:- wakati wa manunuzi makubwa(gari, nyumba), familia yenu iwe na watu wangapi?, Shule/Malezi ya watoto na pengine “career”.Unapowakilisha jambo/kero kwa mwenza wako ni vema kuwa katika hali ya utulivu(sio mara zote hufanya kazi hasa kama mwenzio sio msikilizaji mzuri). Utulivu wako husaidia kutoongea kwa sauti ya kushambulia na hivyo kuepeuka yeye kujitetea(bila shambulio hakuna pa kurudisha shambulio).Unapoibua suala ili lizungumzwe/jadiliwe nia ni kufikisha Ujumbe/kero na kupata muafaka(maelewano) na sio kung'aka na kuanza kugombana....hii hupoteza muda(kusumbua watoto kihisia/akili) na tatizo kuzimishwa badala ya kumalizwa.Kuzima/acha tatizo bila muafaka/maelwano kwa muda mrefu hupelekea mwanzilishi wa “mazungumzo" kuhisi kuwa hasikilizwi na hisia zake hazithaminiwi na mwenza wake.Hisia hizo hupelekea hasira(jitahidi kujizuia ili usifanye jambo mbaya) na pengine kupunguza Heshima kwa mwenza wake.


Kutoelewana/sikilizana pia hupelekea “issues" kurundikana kitu ambacho sio afya kwenye Uhusiano wenu.Suala muhimu hapo ni Msikilizaji ambe hakusikiliza na badala yake kuanza kujitetea kwa kung'aka(na kutimia maneno  makali ya kuudhi) kuomba radhi.Siku nyingine, jaribu kuomba mzungumze na kumwambia mwenza wako kuwa “naomba tuongee kuhusu blablabla, usikilize kwanza mpaka mwisho bila kufoka, kujibu wala kunikatisha.Heshima ikikosekana kwa pande zote mbili, Uhusiano unaweza kuyumba na pengine kufa. Heshima ni Moja ya Nguzo muhimu. Njoo tena ukipata muda, tuiangalie Heshima kwa “engo” tofauti na ile ya 2015.....Muda wako unathani kubwa kwangu, ahsante.
Bai.

Sunday, 15 August 2021

Nguzo 5 za Mahusoano/Ndoa Bora...

Nguzo 5 za Mahusiano bora ya Kimapenzi ilikuwa topic maarufu sana 2007. Unakumbuka?


Nilizielezea kwa kirefu kama utambulisho, wakati ule wengi walikuwa hawafahamu na baadhi hawakuwa wameziishi.


Sasa tangu umeziishi nineona sio mbaya kama nikizirudia tena kwa pembe tofauti kidogi na ile ya 2007.


Kabla sijaenda huko hebu nikukumbushe Nguzo hizo ambazo ni...

1) Mawasiliano.
2) Maelewano/sikilizano
3) Ushirikiano
4) Heshima
5) Kujali


Ni rahisi kudhani kuwa wewe na Mwenza wako mnafanya yote hayo na kuamini kuwa Uhusiano wenu upo Imara.


Utajuaje kuwa Mawasiliano ni mabovu?

Mara ya mwisho kukaa chini na kuzungumza masuala yenu binafsi na yale ya kimaendeleo?


Je, mwenzako anapokuja na hoja, huwa unasikiliza, jadili inapobidi na kufikia maelewano? 


Ikiwa Mara zote mnaishia kubishana badala ya kujadili sababu mmoja wenu kapandisha sauti(foka) basi ujue uhusiano wenu hauna mawasiliano.

Ni muhimu kutafuta namna ya kurekebisha na kuboresha kona hiyo.

Njoo tena tuseme kuhusu Masikilizano kwa pembe tofauti na ile ya miaka 14 iliyopita. 

Nathamini Muda wako, ahsante. 

Bai.

Tuesday, 10 August 2021

Uviko nusura uue Viungo vya Uzazi...

...umesikia mengi kuhusu mabaya ya Uviko kuanzia upumuaji, vifo, ukosefu wa pesa/kazi, mpaka ongezeko la kuvunjika kwa Ndoa(Talaka).

Inaonekana wanandoa wengi walikuwa hawajuani, sasa baada ya kulazimika kukaa pamoja masaa 24 kwa zaidi ya miezi 3 wakagundua Wenza wao sio Wenza wao tena.


Mf;  kwenye baadhi ya Ndoa wamegundua hakuna mawasliano kati yao. Au Mume kapoteza "value" sababu  sehemu ya majukumu yake (kulinda, kutunza/lisha) yamechukuliwa na Serikali.


Hata kama Mke alikuwa "working mama" kabla, Majukumu yake kwa kiasi kikubwa yatabaki palepale. Tofauti na mwenza wake.


Hakuna kitu kinaondoa mvuto kama Mwanaume kutokuwa na Shughuli ya kumuingizia Pesa...hii hupelekea kupoteza takwa lamwili na hivyo ukosefu wa Tendo na hivyo watu wakaanza kushi kama "housemates" na sio wanandoa.


Kwabaadhi yetu hali haikuwa mbaya hivyo, sema tatizo lilikuwa Vitakasa mikono. Kwasababu ya uoga(na uvivu wa kwenda kunawa mikono kwa maji na sabunu mara kwa mara) matokeo yake unapeleka mikono "kunako" kunogesha hisia...kesho yake unaanza kuwashwa sirini.


Unajiuliza Jamaa kaniletea gonjwa la zinaa? Ila kalipataje na tuko pamoja 24/7 mwezi wa 9 huu. Kumbe ni "irritation" ya Vitakasa Mikono.

Nathamini muda wako, ahsante.
Bai.


Monday, 9 August 2021

Miaka 3...

....siku 3(tangu niingie humu) na watoto 3 later.  Natumaini unaendelea vema na lolote ufanyalo ambalo ni Chanya.


Ndani ya miaka hiyo  mitatu mengi yametokea iwe ni Mahusiano mapya, Kuuguza, Ndoa, vifo na uhai mpya.  Ni matumaini yangu kuwa matukio hayo kwa namna moja au nyingine yamesaidia katika ukuaji wako na kuona Maisha yalivyo tofauti upande wa pili.Mimi binafsi sipendi kuzungumzia, soma au angalia mambo Hasi kama njia ya kujipunguzia mawazo kwa vitu visivyonihusu.


Inawezekana wako ikaonekana kama ni ubinafsi "kutokujali"  watu na matatizo yao...ila ukweli ni kuwa sote tunamatatizo nje ya Mitandao.


Na naamini kwa kila mmoja wetu, sote tunapambana na kukabiliana na matatizo yetu na wapendwa wetu...hivyo sio busara(wala Afya) kufuatilia matatizo ya watu wengine.


Nimesema hayo ili nikuambie kuwa, ukizidiwa na mataizo ya watu njoo hapa tukumbushane, tucheke na kujifunza jambo. 


2021 sitokuwa naandika sana ili nisikuchoshe ila nitaandika mara kwa mara ili nisikupoteze.

Tambua nathamini muda wako na ahsante.
Bai!