Huwezi kuwa Mke bora ikiwa hufanyi mambo Milioni moja na nusu ikiwa ni pamoja na Kujali.
Kujali kwenye Ndoa sio kitu kinachotakiwa kufanywa na Mke, bali Mume pia. Japokuwa kwenye jamii Mke ndio hutegemewa kuonyesha kujali zaidi kuliko mwenza wake wa kiume.
Mke atahakikisha Mume analala mahali safi na comfortable, nyumba safi na inapendeza, Nguo na hata Chakula kimeandaliwa vema na kwa wakati.
Mke hatoishia hapo, atajiswafi na kujiremba/pendezesha/nukia vizuri kwa ajili ya Macho na Heshima kwa Mume(watu watakao kuona nje).
Mke ataendelea kutoa ushari, kumtuliza, kumpa moyo/matumaini, kum-support, kuhakikisha ana Afya njema na kumkumbusha suala zima la kuilinda Afya yake.
Ikiwa mnaishi mbali na Wazazi wa Mume, Mke atakumbusha kuwajulia hali na pengine kwenda kama Familia ili wasipoteze ukaribu kwako na Wajukuu zao.
Mwisho kabisa, Mke atahakikisha watoto wanakubuka siku Muhimu kwa Baba yao na kukupatia vijizawadi kwa niaba yao(Watoto)
Uliza Mumeo anakujali kwa
kufanya nini? Kwa 99% atasema “naenda Kazini kila siku ili kulinda na kulisha familia yangu”.
Hutofurahia hilo jibu kwasababu huko sio kukujali bali kutimiza Wajibu wake kama Mume....maana na wewe(pengine Dada wa Kazi) unalinda, tunza, lea, fundisha watoto wenu.
Unajua kwanini Mumeo hajali kama unavyojali wewe?
Ni kwasababu Mwanaume haandaliwi kuwa Mume bali Mhudumia familia iwe Wazazi wake ama wadogo zake, ntugu na jamaa.
Ili mumeo aonyeshe kukujali inabidi uwe wazi na kumwambia ni nini hasa unataka akufanyie nini?
Comments