Skip to main content

Posts

Showing posts from November 15, 2015

Era ya Kulazimishana ku-react!

Heiyaaa! Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia  unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k. Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe. Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k. Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe&

Wasichana tuliokulia miaka ya 90...

....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao. Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90. Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza  miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).