Heiyaaa!
Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k.
Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe.
Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k.
Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe" (waliokuwemo kitambo kwenye Sosho Midia) kulazimishana ku-react na matokeo yake utakuta kila Blog/Site inazungumzia tukio lile lile kwa Siku kadhaa......kama ilivyo kwenye News Media. Sasa pengine Blog wanakimbiza "traffic" kwa sababu za kimapato zaidi na sio kwamba wanajali,umia au chukizwa na tukio fulani lililotokea.
Platform kama Twita na Facebook zimekuwa zikitumika kulazimisha watu wa-react au ku-fit in na kuonekana(hata kama hawana hisia hizo) kuwa wameumia na wanajali kuhusu Tukio fulani linaloendelea kwa wakati huo.
Nitakupa Mfano mwingine. Linapotokea Shambulio au Maafa kwa Nchi kama India, Nigeria,Pakistan, Palestine, Ukrain, Russia na Israel huwa sipati hisia yeyote(nimechoka kusikitika na kukasirika), huwa si-react(nakuwa kawaida tu)....sasa silazimiki kuungana na wale walio-react kwa furaha au hasira au chuki na huruma......Hisia hailazimishwi, inajitokeza tu yenyewe.
Ikitokea umeguswa na tukio, usianze kuhamishia hasira zako kwa watu wengine na kuwalazimisha waungane na wewe au na ninyi ili "kuonyesha" kuguswa sawa wakati wanajua kabisa hawajakuswa kama ulivyoguswa wewe.
Imefikia mahali mtu unaamua ku-fit in ili uwe-protected na Magwiji uliowakuta kwenye hiyo Sosho Midia, kwamba ukienda tofauti na mtu na ukawa-attact maGwiji wanakuja kukusaidia. Umezoea ku-fit in mpaka unapoteza uwezo wa kujitetea. Ukiwa mtaani ana kwa ana na attacker au bully utafanya nini?
Labda tujaribu kuacha Kacha ya kutaka # zetu ku-trend kwenye Sosho Midia na hivyo ku-bully wenzetu ili wa-fit in na vile tunavyohisi sisi. Kila mtu ana haki ya kuweka/kutokuweka Hisia zake wazi, japo ni muhimu kuzingatia Sheria za unapoishi ikiwa unataka ku-share Hisia zako ambazoo ni Hasi. Tukubali kutofautiana iwe Kijinsia, Kiuchumi, Kihisia na mengineyo.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments