Skip to main content

Posts

Showing posts with the label jamii

Hii ndio sababu ya mawifi/Mama wake kutuchukia?

Usinielewe vibaya, mie pia ni Wifi "mkubwa", lakini  tofauti ni...sio  kwamba nawachukia(hawajawahi kunikosea) au nawapenda(sijawahi kuishi nao).....nawachukulia kama walivyo na kuwaheshimu kama wanavyoniheshimu. Kamwe sijawahi/siwezi kujaji lolote kuhusu wao kwasababu siwajui kama ambavyo Kaka zangu wanawajua Wake zao. Sijawahi kuhoji kwenye  kufanana kwao na watoto wao. Huwa nasema tu mnawatoto wazuri, wapwa wangu wanapendeza n.k. Ikiwa Kaka zangu hawakuwa Makini na wanalea watoto wa wenzao, hiyo ni issue yao, sio yangu. Sasa, kuna siku nilikuwa nazungumza na Asali wa Moyo wangu kuhusu mambo ya Kijamii na tukagusia Chuki ya Wanawake kutoka Upande wa Mwanaume, akaniuliza hivi ni kwanini? Nkamwambia mie pia ni Wifi(mwanamke kutoka upande wa Kaka zangu) lakini sina Chuki na wala sifuatilii mambo yao na familia zao! Tukaenda ndani (deep)kidogo, nikagundua kuwa, chuki hii inaweza kusababishwa na moja9au yote) kati ya haya yafuatayo;- *Mwanamke anajua kuwa yeye ni

Era ya Kulazimishana ku-react!

Heiyaaa! Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia  unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k. Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe. Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k. Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe&