Ni Ijumaa nyingine tena ambapo tunaendelea na "Series" yetu. Unakumbuka nilikuambia kuwa pale Shuleni kwangu kwa zamani kulikuwa na Watoto wa watu Wazito na wale wa Mabalozi wa Tz Nje(waliokuwa wanasubiri kupewa Ofisi).....Tulipokuwa Kidato cha Pili kikaja kimtoto kina miaka Nane kilikuwa kinatokea Nchi gani sijui huko. Kilikuwa kinashuka mahisabati kwa Kiingereza hicho hihihihihihi. Aliondoka baada ya Wiki 6. anyway. Kusoma na watoto wa watu wazito ni raha, unapata kujua mambo mengi sana kuhusu maisha yao na(sio muhimu kivile lakini ndio hivyo), unakula maCandy na Majuisi ya Ulaya bana.....hasara yake inakuja kwenye Mitihani, sio siku ya Mitihani bali kwenye Matokeo. Kama unakumbuka mwaka wetu(piga mahisabati mwenyewe) baada ya Matokeo kufutwa(sote tukafaulu) ndio Mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili ukafutwa, sababu zilikuwa nyingi kwanini hakukuwa na umuhimu wa Kukaa Mtihani wa Kidato cha Pili. Nakumbuka siku tunaenda kuangalia Matokeo(ilikuwa siku ya s