...enzi za DHB, Yahoo/MSN chatrooms (heeey Maajuza wenzangu hihihihi) ilikuwa ni kawaida kuulizawa upo wapi na unafanya nini au umefikaje huko uliko, wengine wanapitiliza mpaka kwenye unakuja lini Bongo n.k. Kwa baadhi yetu ilikuwa sio big deal kwasababu info hazikuwa muhimu kivile(kabla ya Google haijatufanya Kijiji) kuorodhesha Nasoma, mwaka wa pili na huwa narudi Home kila Christmas.
Jisni siku zilivyozidi kwenda na Maendeleo kuongezeka na watu wengi kuwa na wasaa wa kufikia Mitandao na hivyo kuweka mengi kuliko wanavyohitajika. Siku hizi imefikia mahali wewe mwenyewe kwa hiyari yako unahisi kusema/share kila kitu, ikitokea mtu kauliza basi unajimwaga kwa uhuru kabisa, which is okay maana info ni zako bwana. Tatizo ni kwamba wengi mnatoa mengi kuliko mnavyohitajika na matokeo yake baada ya muda wale wale mliowaambia wanatumia hayo kukuumiza au kukudharau.
Hakika kila mtu ana haki ya kusema atakacho kuhusu maisha yake Halisi au ya Kimtandaoni ili tu awemo anapotaka kuwemo,,...hali ambayo inaweza kukupa Presha ku-keep up au ku-maintain Mtindo huo wa Maisha uliojitengenezea Online au ule ulioaminisha watu. Hali inayoweza kukusababishia dharau ikiwa wale "uliowaaminisha" wakukute unaishi vinginevyo(wapate kujua ukweli).
Pamoja na kuwa ni uamuzi wako na ni haki yako kusema/share kila jambo lako, kumbuka kuwa sio lazima. hulazimiki by Law kufanya hivyo, kwahiyo zingatia nini hasa unataka kuweka wazi na nini kibaki kwa ajili ya watu wako wa Karibu na Marafiki(kama unao) waaminifu.
Kwasababu tu wengi ulionao kwenye maisha yako ya Mtandaoni(kwenye Sosho Midia) hasa maCeleb wanaweka kila kitu(wapo kazini na wanalipwa kufanya wafanyavyo) haina maana na wewe pia ufanye hivyo.
Ku-share kupita kiasi huenda mpaka nje ya Mitandao/Sosho Midia. Mfano baadhi yetu huwa na tabia ya Ukarimu eeh Watanzania sie ni ndugu. Jamaa kutoka Serikalini anakuja Ughaibuni kwa mfano, anataka kutunza Pesa alizopewa kwa ajili ya Hotel.....anatafuta connection ya mtu mwenye nyumba kubwa ampe Chumba ili a-save anunulie familia ya Mazawadi ya UK au akajenge huko Bongo baada ya Semina.
Unapomkaribisha mtu kwako(akae bure au achangie sehemu ya Bill) na kuishi nae kwa muda wa siku 3 au zaidi hakika atakuwa amekusanya Info za kutosha bila wewe kukusudia kuzitoa na matokeo yake anazitumia hizo kujumuisha Watanzania waishio Nje na hapo ndio Dharau inapoanza.
Kuanzia sasa Muache kukaribisha Wabongo kwa kisingizio cha Ukarimu/sisi Ndugu majumbani mwenu wanapokuja kwa ajili ya Semina, waacheni wakakae Hotelini huko. Hao mnaowafanyia Wema ndio hao hao wanaokwenda kuwaumiza na matokeo yake wote tunaonekana tunaishi maisha ya Kishenzi mnayoishi nyie......duh! hii sijui imetoka wapi.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Comments