Friday, 30 October 2015

Kufutiwa Matokeo Kidato cha 2.....Miaka 20 Tangu Secondary!


Ni Ijumaa nyingine tena ambapo tunaendelea na "Series" yetu. Unakumbuka nilikuambia kuwa pale Shuleni kwangu kwa zamani kulikuwa na Watoto wa watu Wazito na wale wa Mabalozi wa Tz Nje(waliokuwa wanasubiri kupewa Ofisi).....Tulipokuwa Kidato cha Pili kikaja kimtoto kina miaka Nane kilikuwa kinatokea Nchi gani sijui huko. Kilikuwa kinashuka mahisabati kwa Kiingereza hicho hihihihihihi. Aliondoka baada ya Wiki 6. anyway.

Kusoma na watoto wa watu wazito ni raha, unapata kujua mambo mengi sana kuhusu maisha yao na(sio muhimu kivile lakini ndio hivyo), unakula maCandy na Majuisi ya Ulaya bana.....hasara yake inakuja kwenye Mitihani, sio siku ya Mitihani bali kwenye Matokeo.

Kama unakumbuka mwaka wetu(piga mahisabati mwenyewe) baada ya Matokeo kufutwa(sote tukafaulu) ndio Mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili ukafutwa, sababu zilikuwa nyingi kwanini hakukuwa  na umuhimu wa Kukaa Mtihani wa Kidato cha Pili.
Nakumbuka siku tunaenda kuangalia Matokeo(ilikuwa siku ya shule) wanafunzi wengi hawakuona Majina yao pale kwenye Karatasi za Matokeo, watu wakaanza kulia eeh bana(nani anataka kurudia Kidato?)....hao kwa mwalimu Mkuu. Mwalimu akaanza kupiga simu huku na kule.

Baada ya siku tatu Majibu yakaja na wote ambao hawakuona majina yao kwenye Karatazi za Matokeo, wakawekwa kwenye karatasi mpya, lakini wote wakawa wamefeli! Vita si ikaanza bwana, wazazi wakaja juu hawakubali kuwa Watoto wao wamefeli. waliamini kuwa Wamefelishwa ili Watoto wa Wazito wafaulu.
Ile mbinu ya kawaida ya Walimu wa Shule ya Msingi kwamba  Mtoto wa Mwalimu akifeli  basi  Mtihani lazima urudiwe!  ilishindikana kwasababu Mtihani uliandaliwa Kitaifa. Wakaona isiwe tabu basi wote mmefaulu na hakutakuwa na Mtihani wa Kidato cha Pili....hihihihihi. Nadhani waliurudisha baada ya Mwaka au miaka miwili baadae.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.

babai.

No comments: