.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini.
Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi).
Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) bali unachukia kwasababu unahisi au kudhani kuwa unafanana nae kwa namna moja au nyingine.
Kuna wadada hufurahia sana kuambiwa na wapenzi wako kuwa Umefanna sana na Ex wangu(yep nawafahamu wengi tu) kwasababu tu Exs walikuwa Hot......inasikitisha lakini ndio ukweli kwa baadhi ya sisi Wanawake.
Wengine hudhani kuwa wanawake huwachukia Ex wa wapenzi wao kwasababu waliwatangulia na hivyo wao kula Makombo.....hii sababu ni invalid kwasababu Kimaumbile mwanaume haachiwi uchafu na kukaa nao kwa muda mrefu(unless alipata Gonjwa) pia Mwanaume hazai na hivyo hata kama alizaa na Ex wake bado huyo mwanaume sio Makombo.
Ex wake kwa next mpenzi ndio atakuwa anakula makombo hasa kama ex(mwanamke) huyo ameachana na mtu wake chini ya Miezi 3 au alizaa nae, alipoingia akaacha Uchafu wake kisha ukatoka kama Mtoto na yeye ndio anaenda hapo hapo(rejea Topic ya Usiku Mmoja).....samahani hii haina Mfumo Dume hivyo usiingize U-Feminis hapat...... ni Fact of Life.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments