Skip to main content

Posts

Showing posts from October 4, 2015

Eating Clean: Kifungua Kinywa kwa busy mums

Kama wewe ni busy Mum wa watoto wawili chini ya Miaka Mitano bila Msaidizi kama mimi,  hakika utakuwa unatafuta Kifungua kinywa kitakachokaa tumboni muda mrefu.  Chakula kitakachokuchukua kuanzia saa Moja asubuhi mpaka saa Kumi na Moja Jioni(au muda wako unaokula Chakula cha jioni/usiku). Hapo katikati unaweza kutafuna chochote na kunywa maji (ya kutosha) ili kujiongezea nguvu na kukata Kiu ila hutopata hisia ya kutaka kula chakila kizito. Baada ya kujifungua mtoto wa pili nilikuwa nakula Lunch asubuhi na nilifanikiwa kupunguza Mwili wa "Mimba".....then nikagundua Mayai na Kale (mboga jamii ya Kabeji). Nadhani ni kama Spinach(sio Mchicha kama Wanavyoita wa UK na US), unazijua zile Spinachi tulikuwa tunapanda kwenye Bustani za Shuleni(kama ulisoma Shule za Msondo aka non Academy? Radha yake na Muonekano wake ni tofauti lakini nahisi kuwa ni Jamii hiyo. Kwa kawaida nakula Mayai 3(kiafya unajitaji 2 kwa siku)....huwa nachanganya na Kale  kisha na

Kipindi cha Baridi ndio unahisi kuwa Stylish....

Jambo! Nimeamua kuipenda Autum/Winter sasa, sio tu kuwa Kipindi hiki ndio najihisi kuwa stailishi bali pia napata nafasi ya kutumia(vaa) kila aina ya nguo niliyonayo kwa Kujiamini zaidi kwasababu hakuna  ile "presha" ya Kunyoa Kwapa wala Miguu na Mikono.....(well naficha chini ya Tights, Jaketi au Koti). Halafu Majira haya ni Marefu kuliko hizo siku 3 za Kiangazi. September Mpaka June ni total Baridi. mekosa Pic ya Mweusi ambae ana-stayle kama yangu (ubaguzi kando) Halafu pia Wivu wa hali ya hewa unakuwa hauumi sana kwa walio  Nchi za joto, unajua kuna muda unaangalia Fashinblogs za Tz halafu unapata Wivu wa hali ya hewa.....wanavalia nguo nyepesi na wanafurahia Kiangazi kwa Muda mrefu zaidi yako. Kipindi cha Kiangazi huku kinadumu kwa Mwezi mmoja, tena sio Mwezi Mzima mnapata Jua la maana bali mara mbili au tatu kwa Wiki ndani ya Miezi 3! Sasa kuna ulazima gani ya kuipenda Summer(Kiangazi)? Halafu huku tulikohamia Mwaka huu Kiangazi kilijitokeza kwa Si

Dawa za Kuzuia Mimba.....Ukweli uliofichwa!

Haiyaaa! Kitambo eti? Leo tuzungumzie Dawa za Kuzuia Mimba, pengine unajua Mengi kuhusu hili zaidi yangu kwa sababu mie sijawahi kuyatumiaga haya Makorokocho bana. Sababu kuu haikuwa kwamba niliogopa Saratani (zote zinaongeza Uwezekano wa kupata Cancer), au Kunenepa(inategemea na Mlo wako) au kukonda bali sikutaka kuwa "mchafu"......Napenda Ngono sana tu ila sina Mpango wa Kuolewa na Wewe wala kuzaa na Wewe sasa kwanini unikojolee(achie uchafu wako, wakati wangu unauosha in sekunde). Mara nyingi huwa nakuwa Mkali ikiwa Binti(well mdogo wangu) ananijia na kuniomba ushauri wa kutumia Dawa za kuzuia Mimba wakati hana mpango wa kuolewa na huyo Bf wake.....nkauliza utakojolewa na wangapi in your life wajameni??!! Pia huwa naudhika ninaposikia Wanaume wanasema kuwa ni kazi ngumu sana kumalizia Nje na Condom inapunguza "utamu" na hivyo kuwasukuma/Lazimisha Wanawake kwenda na kutumia Vidonge/Sindano au kufanyiwa "upasuaji mdogo" ili kuwekewa ile "Y

Maharage Mabichi kutoka Tz yauzwa ASDA-UK

Unajua ile furaha unayipata unapokula kitu kutoka kwenu ambacho hujawahi kukila ulipokuwa kwenu? Kwamba unakula kwasababu tu unahisi unampa sapoti Mkulima wa kwenu. Hii ni mara ya tatu nanunua bidhaa hii  kutoka Asda kwasababu kuu mbili. Moja ni ya kijani(sababu za kiafya na kutunza mwili) na pili ni kwasababu yanatoka Bongo. Jinsi ninavyotengeneza: (kama upo interested)... Kula na/kwa Wali kama mboga: Nayachemsha kwa sekunde kiasi kisha namimina Tui la nazi (well unga wa nazi uliochanganywa na maji ya moto). Ongezea utamu kwa mlo wako kwa kuweka Embe mbivu au Ndizi mbivu. Kula na Samaki bila Wanga: Nayachemsha  pamoja ya "maua ya coli" na "brocoli" kisha  nanyunyizia pilipili Manga na Chumvi kisha namwagia "Fish sauce" kama uonavyo picha na tuvipande twa  Samaki. Kama ni mpenzi wa Rost pia zinakwenda vema hakikisha una Gravy. Unaweza kuchanganya hizo na Kisamvu (kuungwa na Karang