Kama wewe ni busy Mum wa watoto wawili chini ya Miaka Mitano bila Msaidizi kama mimi, hakika utakuwa unatafuta Kifungua kinywa kitakachokaa tumboni muda mrefu.
Chakula kitakachokuchukua kuanzia saa Moja asubuhi mpaka saa Kumi na Moja Jioni(au muda wako unaokula Chakula cha jioni/usiku). Hapo katikati unaweza kutafuna chochote na kunywa maji (ya kutosha) ili kujiongezea nguvu na kukata Kiu ila hutopata hisia ya kutaka kula chakila kizito.
Nadhani ni kama Spinach(sio Mchicha kama Wanavyoita wa UK na US), unazijua zile Spinachi tulikuwa tunapanda kwenye Bustani za Shuleni(kama ulisoma Shule za Msondo aka non Academy? Radha yake na Muonekano wake ni tofauti lakini nahisi kuwa ni Jamii hiyo.
Kwa kawaida nakula Mayai 3(kiafya unajitaji 2 kwa siku)....huwa nachanganya na Kale kisha naweka kwenye Microwave kwa dk 3. Halafu nanyunyizia chumvi na pilipili Manga. Nakula na tunda Moja.
Huwa nabadilisha matunda kati ya Apple na Ndizi Mbivu au Embe Mbivu. Siku nyingine nabadilisha "upishi"......badala ya kuMicrowave huwa nakaanga kwa kiasi kiduvhu cha Olive oil na kisha naongeza Jibini kwa juu(kabla Yai halijapoa).....kama picha inavyoonyesha.
Mwili wako unahitaji Protein kama mwanamke kwa ajili yakujenga Misuli(kama unazoezika) na Kale ina Vitamins na Mineral muhimu na inasaidia Nywele na kucha zako kuwa na afya njema na kukua haraka kuliko kawaida yake.
Mabadiliko ya mwanamke baada ya kuzaa ni mengi higyo ni vema kuwa muangalifu na unachokiweka au kukiondoa mwilini. Mlo huu haukinai (mwaka wa pili na nusu nakula hivyo kila Asubuhi) na haunenepeshi so long unakula mlo huu mara moja Kwa siku. Na usile mlo mwingine uliopikwa kwa kutumia Mayai.
Naheshumu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.
Babai.
Comments