Skip to main content

Posts

Showing posts with the label afya

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......

....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini? Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu. Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Ha

Eating Clean: Kifungua Kinywa kwa busy mums

Kama wewe ni busy Mum wa watoto wawili chini ya Miaka Mitano bila Msaidizi kama mimi,  hakika utakuwa unatafuta Kifungua kinywa kitakachokaa tumboni muda mrefu.  Chakula kitakachokuchukua kuanzia saa Moja asubuhi mpaka saa Kumi na Moja Jioni(au muda wako unaokula Chakula cha jioni/usiku). Hapo katikati unaweza kutafuna chochote na kunywa maji (ya kutosha) ili kujiongezea nguvu na kukata Kiu ila hutopata hisia ya kutaka kula chakila kizito. Baada ya kujifungua mtoto wa pili nilikuwa nakula Lunch asubuhi na nilifanikiwa kupunguza Mwili wa "Mimba".....then nikagundua Mayai na Kale (mboga jamii ya Kabeji). Nadhani ni kama Spinach(sio Mchicha kama Wanavyoita wa UK na US), unazijua zile Spinachi tulikuwa tunapanda kwenye Bustani za Shuleni(kama ulisoma Shule za Msondo aka non Academy? Radha yake na Muonekano wake ni tofauti lakini nahisi kuwa ni Jamii hiyo. Kwa kawaida nakula Mayai 3(kiafya unajitaji 2 kwa siku)....huwa nachanganya na Kale  kisha na

Come to terms with your Uchibonge....

Hello! Naweka viraka mbinguni ujue(mekuwa busy namna hiyo). Mwisho wa wiki nilipata wasaa wa kupekua pekuwa YouTube na huko nikakutana na "how to gain weight".....nikabofya na kuanza kusikiliza hadithi moja baada ya nyingine kuhusu Wanawake wanaotaka sana kunenepa. Unajua unapomsikiliza mtu au kusoma hadithi yake na kuhisi kuwa anakysemea au kukuwakilisha wewe? Yaani anakugusa kumtima. Nikakumbuka jinsi nilivyokuwa Chikonda (skinny)enzi zile nakua(nimeacha kukua nilipofikisha miaka 25 nadhani). Story Time: Nilikuwa mwembamba kiasi kwamba baadhi ya watu walidhani nina Ugonjwa. Mmoja wa Binamu zangu alikuwa akiniambia "mtu mwenyewe maiti wewe.....umebaki mifupa tu". Nilipofika late teen baadhi ya watu Familiani wakawa wanasema ninatoa mimba sana wakati sikuwa namjua mwanaume sasa sijui Mimba ziliingia kwa Roho mtakatifu! Wengine walisema naiga Uingilishi figa na hivyo kutumia madawa ya kujikondesha. Nilichoka kusakamwa kwa uchikonda wangu ambao sikuuom