Skip to main content

Come to terms with your Uchibonge....

Hello!

Naweka viraka mbinguni ujue(mekuwa busy namna hiyo).


Mwisho wa wiki nilipata wasaa wa kupekua pekuwa YouTube na huko nikakutana na "how to gain weight".....nikabofya na kuanza kusikiliza hadithi moja baada ya nyingine kuhusu Wanawake wanaotaka sana kunenepa.


Unajua unapomsikiliza mtu au kusoma hadithi yake na kuhisi kuwa anakysemea au kukuwakilisha wewe? Yaani anakugusa kumtima.



Nikakumbuka jinsi nilivyokuwa Chikonda (skinny)enzi zile nakua(nimeacha kukua nilipofikisha miaka 25 nadhani).



Story Time: Nilikuwa mwembamba kiasi kwamba baadhi ya watu walidhani nina Ugonjwa. Mmoja wa Binamu zangu alikuwa akiniambia "mtu mwenyewe maiti wewe.....umebaki mifupa tu".



Nilipofika late teen baadhi ya watu Familiani wakawa wanasema ninatoa mimba sana wakati sikuwa namjua mwanaume sasa sijui Mimba ziliingia kwa Roho mtakatifu!


Wengine walisema naiga Uingilishi figa na hivyo kutumia madawa ya kujikondesha.



Nilichoka kusakamwa kwa uchikonda wangu ambao sikuuomba. Nikaanza kunywa Uji wa Ulezi na kula Mayai na kunywa Maziwa kila leo. Kaka yangu akanifundisha mazoezi ya kukuza misuli ili nionekane mnene so nikaanza mazoezi ya kienyeji (kuchutama ili miguu na mapaja  yanenepe, kunyanyua Nondo za 5kg ili ninenepe aka jazia mikono).



Matokeo yake nikawa nanenepa sehemu ya chini kwa nyuma pale kati ya mwili.....so nikawa naonekana mwembamaaa halafu  nimebinuka aka chikonda mwenye tako lililojitokeza.....kikaambiwa naTigoliwa.....Wanadamu bwana daaaah!


Ikafikia mahali nikakubali tu kuwa mimi ni mwembamba so nikawa nafanya mazoezi kwa ajili ya kiafya na sio kunenepa tena.


Nikaambiwa nikizaa nitanenepa na kweli nilinenepa in which sikupenda Unene ule kwasababu sikuzoea kuwa Mnene so nikajitahidi na kurudia size yangu ya awali mara tu baada ya kujifungua.


Baada ya mtoto wa pili naona mwili hautaki kurudi pale 8-10.....nimefanya yote sahihi kwa Miaka miwili ili nirudie size yangu lakini wapi.


Sasa nimekubali AGAIN kuwa mimi ni chibonge sio kiviiile bali size 10-12. Will try and keep this sitaki kurudi size 14....*Size zote ni za UK.


Mimi mkimama wa kawaida (sio Celeb) nilitaka kupungua kwa sababu sikuzoea kuwa "mkubwa" sio kwasababu nilitaka niwe kama one of the Celebs.


Pamoja na kusema hivyo ni vema kuzoezeka na kula kwa juzingatia afya....sio kula makorokocho na Chips.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao