Mabaharia.....I see ya!
Mambo vipi lakini(i sound like a male)? Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Ujue huku nje ya Tanzania kila mtu anauchungu wa maisha kivyake kutokana na sababu zilizomleta....sio mnatujaji kwa kutujumuisha bana.
Kuna wale walikuja kuongeza Elimu ili wakirudi waitumie ilimu yao ya kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yao Tukufu Tanzania.
Halafu wapo waliochukia maisha yao yalivyokuwa Bongo na kwa hasira kutaka kwenda kujaribu au kuanza upya huko kwingine.....hawa kurudi sio chee(as in rahisi).
Wengine walipelekwa na Wazazi wao baada ya kuanza tabia mbaya na zenye kutia aibu Wadhifu....sasa ili Wazazi waendelee ku-keep Status.....er ya Uchungaji wa Kanisa, Ukuu wa Jeshi au Uwaziri n.k so unapelekwa Nje ukafanye Umalaya wako kwa nafasi.
Pia kuna akina sie tulioletwa huku kama Mtaji au Urithi.....kwamba Wazazi wanatumia Akiba ya familia ili ukasome na ukimaliza na kuanza kazi ama ulipe Deni na Riba au uwasaidie Nduguzo ambao technically umetumia Mgao wao wa Urithi ili upate Elimu ya Nje.
Nisiwasahau wale walioamua kuingia Mtini baada ya Kualikwa kwa ajili ya Sherehe au walikuja kimichezo mfano Michezo ya Jumuiya ya Madola na wale waliowafuata wake au waume au wapenzi wao.
Halafu kuna Mabaharia.....hawa bana wamefika Uingereza kwa mfano....kwa kutumia Boti sijui Mtumbwi,Basi au Treni....kivipi? Piga mahesabu mwenyewe.
Wote tunaishi Ughaibuni lakini hasira za Maisha na bidii ya utafutaji ni tofauti sana.
Babai.
Comments