Skip to main content

Posts

Showing posts with the label jaji

Wanawake hatupendani....usimbee awe Jaji sasa!

Sina hakika kama hii ni Imani tu au ni kweli, Naturally Wanawake hawanipendi mie binafsi(imagine ningekuwa mzuri sasa!) ila Wanaume wanananipenda(napatana zaidi na Wakibaba kuliko Wakimama). Kuna siku Mfanyakazi mwenzangu akanijia kwenye Dawati langu akanambia "dinah unajua nakuchukia".....mie nkacheka halafu nikamwambia "sio peke yako, nimezoea kuchukiwa na wanawake"....wewe ungesema is because i am Black! Sasa, hii "wanawake hawapendani" ipo kila Nchi Duniani.....kila mtu anaibuka na sababu yake kwanini hasa hatupendani. Baadhi wanadai ni Wivu wa kike(umbile/kupendeza/mafanikio/kuwa na easylife) na wengine wanasema ni mambo ya Homono tu. Mie sio kwamba nachukia wanawake bali sipendenzwi na tabia ya baadhi ya wanawake wanaofanya maamuzi ya Kipumbavu, kama vile kutojikinga dhidi ya Mimba, au kujitegeshea kushika Mimba ili tu waolewe au wapate sehemu ya Kipato ya Mwanaume husika. Sipendi mwanamke ajishushe ili kuonewa kirahisi. Vilevile

Sio wote Ughaibuni tulifika kwa Ndege....

Mabaharia.....I see ya! Mambo vipi lakini(i sound like a male)? Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Ujue huku nje ya Tanzania kila mtu anauchungu wa maisha kivyake kutokana na sababu zilizomleta....sio mnatujaji kwa kutujumuisha bana. Kuna wale walikuja kuongeza Elimu ili wakirudi waitumie ilimu yao ya kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yao Tukufu Tanzania. Halafu wapo waliochukia maisha yao yalivyokuwa Bongo na kwa hasira kutaka kwenda kujaribu au kuanza upya huko kwingine.....hawa kurudi sio chee(as in rahisi). Wengine walipelekwa na Wazazi wao baada ya kuanza tabia mbaya na zenye kutia aibu Wadhifu....sasa ili Wazazi waendelee ku-keep Status.....er ya Uchungaji wa Kanisa, Ukuu wa Jeshi au Uwaziri n.k so unapelekwa Nje ukafanye Umalaya wako kwa nafasi. Pia kuna akina sie tulioletwa huku kama Mtaji au Urithi.....kwamba Wazazi wanatumia Akiba ya familia ili ukasome na ukimaliza na kuanza kazi ama ulipe Deni na Riba au uwasaidie Nduguzo ambao technically umetumia Mgao wao wa Urithi