Skip to main content

Posts

Showing posts from June 11, 2023

Kufananisha/linganisha relationship...

 ,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo? Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza  jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila. Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha  na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbukia)

Mama/Baba wa mtoto wa kwanza, sio wewe wa sasa!

  Unatambua kuwa ulivyo sasa kama mzazi ni tofauti na ulivyokuwa ulipoanza kuwa Mama/Baba? hasa kama watoto wako wamepishana kiasi fulani kiumri, sio tu ni kwasababu wewe na mumeo/mkeo mmkua bali pia uzoefu wenu kama wazazi unabadilika kuendana na umri wa watoto wenu. Sasa hivi unaongea na mwanao wakubwa kama watu "mzima" wenzako kwa kuwasikiliza, kuwaheshimu na wakati huo huo kuwafunza na kuwakumbusha  kuwa wao bado  ni watoto na wewe ni mzazi mwenye urafiki ila sio rafiki yao na bila kusahau kuwakumbushia uliyowafunza awali. Kwa wadogo zao ambao tuseme labda ndio toddlers, hutowalea kama ulivyowalea hao ndugu zake waliozaliwa kabla yake, kwa sababu sasa wewe ni Mjuzi wa malezi, unafanya mambo bila kuomba ushauri wala kuuliza kwa Mama au Dada au vitabu. Hakuna kinachokushangaza kwasababu yote umepitia na kwa jinsia zote mbili, unajiamini balaa. Wiki iliyopita nilipata muda wa kufikiria(surpriiiise I can actully think) jinsi nilivyobadilika tangu nilipokuwa mama kwa mara ya k