Unatambua kuwa ulivyo sasa kama mzazi ni tofauti na ulivyokuwa ulipoanza kuwa Mama/Baba? hasa kama watoto wako wamepishana kiasi fulani kiumri, sio tu ni kwasababu wewe na mumeo/mkeo mmkua bali pia uzoefu wenu kama wazazi unabadilika kuendana na umri wa watoto wenu.
Sasa hivi unaongea na mwanao wakubwa kama watu "mzima" wenzako kwa kuwasikiliza, kuwaheshimu na wakati huo huo kuwafunza na kuwakumbusha kuwa wao bado ni watoto na wewe ni mzazi mwenye urafiki ila sio rafiki yao na bila kusahau kuwakumbushia uliyowafunza awali. Kwa wadogo zao ambao tuseme labda ndio toddlers, hutowalea kama ulivyowalea hao ndugu zake waliozaliwa kabla yake, kwa sababu sasa wewe ni Mjuzi wa malezi, unafanya mambo bila kuomba ushauri wala kuuliza kwa Mama au Dada au vitabu. Hakuna kinachokushangaza kwasababu yote umepitia na kwa jinsia zote mbili, unajiamini balaa.
Wiki iliyopita nilipata muda wa kufikiria(surpriiiise I can actully think) jinsi nilivyobadilika tangu nilipokuwa mama kwa mara ya kwanza na sasa Mama kwa mara ya tatu. Namna nilianza na mwanangu wa kwanza ni tofauti kabisa na nilivyokuwa mama kwa mtoto wa pili na nilivyo sasa kwa mtoto wa tatu na wote watatu kwa pamoja.
Nikaamua kuongea na mwanagu wa kwanza kwa kuuliza swali "hey dogo unajua mama uliene sasa hivi ni tofauti kabisa na mama uliekuwa nae ulipozaliwa?" Dogo akashtuka na kuanza kuwa emotinal(alidhani namaanisha kuwa mimi sio mama yake mzazi), nikagundua nimekosea maelezo. Nikajaribu tena...."nilipokuzaa wewe nilikuwa mpya na hivyo nilikuwa makini zaidi kwako na kwa dada yako kuliko nilivyo sasa kwa Mdogo wako.
Nikaendelea, ulipozaliwa nilikuwa nafanya kazi nje ya nyumbani hivyo nilikuwa sipati muda mwingi wa kukaa wala kucheza na wewe kwasababu nilikuwa hoi bin taabani. Halafu nilipojifungua dada yako nikabadilika tena, nikawa mama kwa watoto wawili wenye umri na jinsia tofauti, hapo nikapoteza ule-umama nilioanza nao kwako wewe mtoto wa kwanza.
"Nikaendelea kuwa mama wa watoto wawili kwa muda mrefu, na kama mama wa nyumbani nikapata muda wa kutosha kuwalea ninavyotaka, kuwatoa nje, kucheza na nyie na kupumzika(wakilala, maana umama hauishi na hauna mapumziko). Miaka karibu nane ikapita kabla mimi na baba yako kuamua kuongeza wa 3, huyu mdogo wako nae kanibadilisha japo sio kwa kiasi kikubwa kwasababu ninyi ni wa kubwa na hivyo umakini umebaki kwenu kuliko yeye, kwa maana kuwa nime-relax zaidi(kwamba wanacheza nae na sometimes wanampa snacks na kumkataza asijiumize/haribu vitu)".
Mwanangu akasema, "aah sasa nimekuelewa mama, kwanini hukusema hivyo mwanzo badala ya kunichanganya na swali lako"? Nikamuomba msamaha. Nikakumbuka siku moja "niligombana" na wazazi kuhusu mdogo wangu ambe ni mtoto wao na walikuwa na mamlaka yote kumshauri kuhusu maamuzi ya maisha maisha yake. Nikasema "mbona mie nilipokuwa ktk umri huo mlikuwa mnikataza kufanya anavyotaka kufanya yeye(mdogo wangu)? Wakanambia kwasababu wewe sio huyu hukuwaki(ni)cheka.
Anyways, nimekuwa Meghan Mackel kwenye Podcast yake, its all about me, me, me and more kilakitu me. Nikutakie siku njema. Bai!
Comments