Hawa walikuwa "my best friends" wangu yaani walifanya lolote kwa ajili yangu....baadhi ya watu walidhani jamaa walikuwa wapenzi wangu.
Naelewana vema na Wanaume kuliko Wanawake, naturally, wanawake hawanipendi (I think like man most of the time) hihihihihi natania, I just don't click kirahisi na watu wa jinsia yangu.
Jamaly nilisoma nae Msingi na wote tukafaulu yeye akaenda Tambaza na mie nikaenda shule moja hivi pale Mjini kati.....Bado urafiki wetu uliendelea Mpaka Chuo.
Tulikuwa tunakaa Dawati Moja (yeah nilikuwa nakaa na Wavulana), tulikuwa tunapishana nafasi ya kuongoza darasa.
Tulikuwa tukisoma pamoja lakini hatukuwa tukikaa pamoja kwenye Mitihani sio wajua ile kupangwa kwa herufi.....still tulikuwa tukibishana ni maswali gani yatatoka kwenye Mtihani usika.
Urafiki na Dave ulianza Kidato cha Pili, na ukaendelea Mpaka naondoka Tanzania karibu miaka 17 iliyopita. Tulikuwa tukisoma pamoja kila tunapotarajia Mitihani japoku...