Biashara ya Vipodozi inapamba faya mwaka hadi mwaka asante Beauty Gurus wa Youtube.....hata mie mpaka Mascara na lipgloss nimeanza kujipaka Foundation siku hizi(well nimeanza kupaka tangu 2004). Enzi hizo mie napaka ilikuwa haiitwi Faundation bana, ilikuwa inaitwa cream to powder au mimi ndio nilikuwa sijui?hihihihihi. The thing ni kwamba most Gurus (nakojifumzia kupaka make up) ngozi zao kama vile haziko sawa. Yaani kuna mmoja siku nilivyomuona bila make up (mambo ya GRWM as in get ready with me) nilaogopa kuendelea kuangalia.....sio kwamba anatisha la hasha! Niliogopa kusikitika na kulia (tangu mekuwa mama nimekuwa way too emotional). Sasa ni mpango wa make up companies kuweka Viasili vya kuharibu Ngozi asilia ili uendelee kununua bidhaa zao na kuficha uharibifu uliopo Ngozini? Najiuliza. Au ni kutokujua kwa baadhi ya watu na hivyo walikuwa hawasafishi Ngozi na kulala na makeups? Pengine ni matumizi ya Vipodozi aka Makeup wakatu ngozi bado haijakomaa? Unajua kuwa Ngozi ni...