Skip to main content

Posts

Showing posts from September 20, 2015

Siri ya Mtoto wa Kwanza, Kati na Mwisho....

Inawezekana Ndugu zako wanaokufuata au uliowakuta(inategemea umezaliwa wa ngapi) sio Damu  moja kwamba  baba na mama yenu ni mmoja. Umewahi kujiuliza kwanini mtu anaendelea kuzaa na mume/mke ambae anamtenda(tereza nje)? au Utakuta Ndoa inamatatizo lakini wanazaa tu kila mwaka....haikuhusu lakini kama Binaadam kiasilia hatuishi Kudadisi na Kujaji. Kiasili Watoto tunadhania kuwa Mama zetu ni "Malaika" lakini bwana mwanamke akiamua kushenzika anakuwa Mshenzi zaidi ya Shetwani, tofauti ni kwamba Wanawake ni wazuri kwenye kuficha siri zao. Akitaka usijue Baba yako ni nani basi hutokaa umjue......akikuaminisha kuwa fulani ni Baba yako basi itakuwa hivyo(ukidai DNA unapewa Radhi hihihihihi). Mtoto wa Kwanza: Binti yupo na anaempenda lakini Wazazi hawamtaki Jamaa aoe.....wanataka aolewe na mtu wao. Binti anaolewa na mimba yake bila muoaji kujua. Pia Binti anaweza kuwa anaendelea na ampendae ili azae nae batoto atakaowapenda kama baba yao, kuliko kuzaa na limtu

Tulionyimwa Komwe....Faida/Hasara zake!

Tufunge na kuomba kuwa na Komwe isijekuwa Fashion kama vile kuwa na Makalio Makubwa. Tutajificha wapi? wewe utakuwa unanyoa manywele yako Usoni ili uwe na Komwe?.....well mie huwa nanyoa katikati ya Nyusi (huwa zinatishia kukutana japo sio nyingi mnaita "fuzz") pia ili kutenganisha Nyusi  na "Mstari wa Nywele" huwa na Nyoa kati kati yake! Pengine hujawahi kugundua kuwa "Hairline" yangu ipo chini hasa sehemu ya pembezoni(zoom time, usiote tu hihihihi). Umbali kutoka Nyusi kwenda kwenye Nywele ni Inchi Moja na Umbali kutoka kwenye Komwe(ambalo halipo) kwenda kwenye Nywele ni Inchi Mbili na Nusu. Kuwa na "low hairline" kuna tofautiana kama ilivyo kwenye Makomwe, tofauti hizo zinafanya baadhi kutaka kuwa na Sura ndefu na hivyo kuondoa Nywele kwa kutumia Njia mbali mbali ili nywele zisirudi(tazama Picha). Mie binafsi tayari ni ba Mdogo(sura ya kiume), sasa nikiachia Nyusi kuungana wajameni si nitasababisha mkanganyo even more(usiche