Skip to main content

Posts

Showing posts from July 6, 2014

Kuvaa Wig!

Nimekugaya eti?!! Well kwani tulisaini mkataba wa mimi kuwepo hapa kila siku? Hihihihi usiache kusoma bana, hebu baki hapa upate stori ya Wig. Ujue kuna siku akili inachoka alafu kunakuwa kama "empty" hivi kichwani kwa ndani, yaani hata yasiyo na maana nayo huondoka basi inakuwa ngumu kidogo kuandika ili ueleweke. Ikifikia mahali unaandika (huku unasoma bila shaka) lakini unahisi hakileti maana....basi tambua kuwa unahitaji Mapumziko kiakili! Anyway.... Wanangu na Baba yao wamelala....Joto limewachosha, maana leo ka' tupo Kisarawe.....achana na hilo. Nimekaa hapa nikakumbuka Wig langu la kujinyonga wenyewe mnaita Curl sijui Karikiti. Kwa kawaida mie sio mvaaji wa hayo mavitu, ila baada ya "issue" ya nywele nkasema ngoja nami niwekeze kwenye "Afro Wig". Siku (2.5yrs ago) nkalivaa, baada ya kutoka Kazini nkaenda Chekechea kumchukua Babuu ....hee! Mtoto wacha alie alafu anaangalia juu (lilipo Wig) hehehehe....nikazuga bana mbele ya Wazungu as walijua nim

Mama yangu alikuwa Kimada!

Uishie hapo hapo!! Najua umekuja mbio hasa kama wewe ni Kimada aka Mwizi au mtoto wa Kimada. Mama yangu alikua Mke wa haki na sote tumezaliwa Ndoani.....alikuwa* kwasababu Baba ni Marehemu, huko Ahera sijui kaoa tena? Roho itaniuma sana nikijua kaoa tena. Anyway. Kuna wale watoto wa Vimada ambao huja na mijisababu kibao ili kutetea Mama zao Vimada au Baba zao Malaya....wengine wanakuja na "Wake wanajibana wakati Vimada wanajiachia miili yao"....wengine wanajifanya wamefanya "Utafiti" na kugundua kuwa Vimada wanajua Mapenzi kuliko wake n.k. Hakuna ku-justfy hapa, kama wewe ni mtoto wa Kimada utabaki kuwa hivyo!! Tena ngoja nikolezee Mama yako ni kamwizi na baba yako ni kamalaya....tuliache hilo kwanza. Hivi unajisikiaje kwa mfano Umeolewa/Umeoa mtoto wa Kimada, yaani Mama mkwe wako ni "mwizi" wa mume wa mtu na huyo Mume(Baba mkwe) ni Malaya.....hihihihihi mie nisingekuwa comfortable yaani ningekuwa nawakwepa m

Kupotea Suna!

Mara ya kwanza kumiliki "SmartPhone" ndio ikawa mwisho wa Mimi kupotea(in my head)....leo 2014 na Tech yote ya Ramani na Gadgets zote zilizopo za "Directions" bado napotea.....Hapo ndio Suna inakuja sasa(sina sababu nyingine). Kwa kawaida nikipotea huwa sioni aibu kumuuliza mtu au kuomba anielekeze....tofauti yangu na wewe ni hivi; huwa sisimamisha mtu yeyote tu, nategea wale ambao sio attractive (at least machoni mwangu). Kwanini nachagua unattractive watu(Wake kwa Waume)? Hata sijui....ila nahisi kama wao ndio wanatoa maelezo vizuri kuliko wale "attractive"....wanakuelekeza utadhani unawatongoza(mie mwanamke, mke na mama nikutongozee nini wee fala...). Naweza nikaenda mwendo mrefu kutoka sehemu niliyopotea mpaka nikutane na unattractive person ndio nimuombe "directions". Nishakuwa stereotyped sana, hivyo wala siogopi kustiriotaipu watu.....ndio maisha...heri umejua kuliko ningekudanganya. Si eti?