Skip to main content

Mama yangu alikuwa Kimada!

Uishie hapo hapo!!
Najua umekuja mbio hasa kama wewe ni Kimada aka Mwizi au mtoto wa Kimada.





Mama yangu alikua Mke wa haki na sote tumezaliwa Ndoani.....alikuwa* kwasababu Baba ni Marehemu, huko Ahera sijui kaoa tena? Roho itaniuma sana nikijua kaoa tena. Anyway.





Kuna wale watoto wa Vimada ambao huja na mijisababu kibao ili kutetea Mama zao Vimada au Baba zao Malaya....wengine wanakuja na "Wake wanajibana wakati Vimada wanajiachia miili yao"....wengine wanajifanya wamefanya "Utafiti" na kugundua kuwa Vimada wanajua Mapenzi kuliko wake n.k.





Hakuna ku-justfy hapa, kama wewe ni mtoto wa Kimada utabaki kuwa hivyo!! Tena ngoja nikolezee Mama yako ni kamwizi na baba yako ni kamalaya....tuliache hilo kwanza.





Hivi unajisikiaje kwa mfano Umeolewa/Umeoa mtoto wa Kimada, yaani Mama mkwe wako ni "mwizi" wa mume wa mtu na huyo Mume(Baba mkwe) ni Malaya.....hihihihihi mie nisingekuwa comfortable yaani ningekuwa nawakwepa mpaka basi....nisingeweza kuwaheshimu hata!




Sidhani kama tungefikia hatua ya Ndoa, lazma ningeingia mtini mara tu baada ya kugundua.....nani anataka kuendeleza Kizazi cha Kimalaya (Baba Mkwe) na Ukimada(Mama mkwe) eti?



Wanasema mtoto hana uhusiano na tabia za Mama na Baba yake ambazo zilipelekea yeye kuzaliwa, lakini hapo hapo uliona wapi Mnazi unazaa Mapapai?




Inaweza isiwe yeye(mme/mke), wakawa watoto mtakao wazaa....aiiii mambo ya kuletewa wajukuu kutoka kwa Vimada/Malaya mie hata sitaki.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao