Skip to main content

Kuvaa Wig!

Nimekugaya eti?!!

Well kwani tulisaini mkataba wa mimi kuwepo hapa kila siku? Hihihihi usiache kusoma bana, hebu baki hapa upate stori ya Wig.


Ujue kuna siku akili inachoka alafu kunakuwa kama "empty" hivi kichwani kwa ndani, yaani hata yasiyo na maana nayo huondoka basi inakuwa ngumu kidogo kuandika ili ueleweke.

Ikifikia mahali unaandika (huku unasoma bila shaka) lakini unahisi hakileti maana....basi tambua kuwa unahitaji Mapumziko kiakili! Anyway....


Wanangu na Baba yao wamelala....Joto limewachosha, maana leo ka' tupo Kisarawe.....achana na hilo.


Nimekaa hapa nikakumbuka Wig langu la kujinyonga wenyewe mnaita Curl sijui Karikiti. Kwa kawaida mie sio mvaaji wa hayo mavitu, ila baada ya "issue" ya nywele nkasema ngoja nami niwekeze kwenye "Afro Wig".

Siku (2.5yrs ago) nkalivaa, baada ya kutoka Kazini nkaenda Chekechea kumchukua Babuu ....hee! Mtoto wacha alie alafu anaangalia juu (lilipo Wig) hehehehe....nikazuga bana mbele ya Wazungu as walijua nimebadilisha Mtindo wa nywele....kumbe sio Zangu!

Kufika garini, nikalitoa Wig langu, nikafunga Kilemba, aiii mwanangu akafurahi.....ili kuhakikisha kama kweli anaogopa Wig, siku nyingine nikalivaa nikiwa nyumbani.


Ayeee! Mtoto alilia mpaka nikaogopa. Basi bwana ikawa mimi na Wig basi, nkalihifadhi Boskini!


Jana nika-google "Afro Curl Wig", zikaja picha na YTvideos, mwanamke nkaanza na Video.....huwezi kuamini!!!


Kumbe nilikuwa nakosea kuvaa Wig langu, sio kwamba lilikuwa linatisha bali nilikuwa nalivuta zaidi mbele kupita "hair line" so likawa linaonekana sio "natural" hivyo nikawa natisha! Haa watu kazini hata wasiniambie....the washenzi hihihihi.

Maskini mwanangu nilikuwa namtisha, yaani mtu ambae alipaswa kumlinda dhidi ya vitisho na hatari ndio____mbaya sana.


Anyway, siku hizi nalivaa Wigi langu inavyotakiwa pale ninapohisi sitaki kusumbua nywele zangu za asilia....well relaxed-asilia (haileti maana lakini umenielewa).


Kuna tofauti kati ya Ushamba na Ujinga, mimi kwenye Wig nilikuwa mjinga, sasa nimejua (najicheka hapa hatari).


Nikutakie mwanzo mwema wa mwisho wa Wiki.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao