Skip to main content

Posts

Showing posts from December 6, 2015

Kutunza Siri ni Wajibu wako....

...well, inategemea na unachokifanya for a living sio! Si unajua ile Kuapa au kuweka sahihi kuwa kamwe hutotoa siri (ujuayo) ya Kampuni/Mgonjwa/Mteja n.k. isipokuwa tu ikiwa Serikali na Mahakama itahitaji. Hello, natumaini Post hii imekukuta ukiwa na afya njema. Mie binafsi naamini kuwa kutunza "siri" ya mtu au watu ni wajibu wako. Kutokana na kile nilichokuwa nikifanya Miaka 8 iliyopita baadhi ya watu walijenga Uaminifu kwangu, kwamba walikuwa huru kuniambia mengi  kuhusu wao na maisha yao. Kwa maana hiyo nafahamu mengi ya watu wengi ambao hatufahamiani. Ile ilikuwa "kazi" ya kujitolea, sijasomea nilichokuwa n akifanua isipokuwa nilitumia uelewa wangu na uzoefu wangu(natambua unalijua hilo), hivyo sikula Kiapo na wala sikutia saini kuwa nitabaki na "siri" za watu Milele(haina maana nitazitoa). Pamoja na kuwa hakuwa "Kazi" bado nilichukulia na ninaendelea kuchukulia kuwa ni wajibu wangu kuto-share chochote kuhusu watu wote walion

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua....update!

Ni Mwaka na Miezi kadhaa tangu nikusimulie kuhusu Nywele zangu za kichwani ambazo ni Relaxed(bila shaka). Sasa, tangu tunamaliza Mwaka nimeona sio mbaya kama niki-share safari yangu ya kuwa na Nywele  tena zenye urefu wa kutosha kutengeneza mitindo na pia zenye afya. Halafu sio mbaya kama nikikutajia/nikionyesha Bidhaa ambazo zimenisaidia kufika hapa nilipofikia. Vilevile nitakuambia ni Bidhaa gani natumia lini na kwa nini(kwenye post nyingine) na nitaambatanisha Picha. Pamoja na kusema hayo ni vema utambue kuwa Bidhaa hizi hazikuhakikishii matokeo kama yangu, inaweza kuwa bora zaidi yangu au usione mabadiliko yeyote. Baadhi ya Bidhaa hizi nilikuwa natumia kitambo, baada ya kuhangaika na kujaribu aina nyingine na kutofanikiwa nikaamua kurudi kwenye bidhaa kutoka Vitale, Nikaamua kutumia "Steamer" na "Blow dryer". Awali nilikuwa situmii Heat kabisa kama nilivyoshauriwa na Gurus. Baadae nikagundua kuwa Nywele zangu zinapenda Heat so nikarudia utaratibu w