Skip to main content

Posts

Showing posts from August 16, 2015

Kwa Mliojipiga/Lipua/Fuata Sheria Ughaibuni....

....yote Maisha na kila mtu anayatafuta kwa namna yake sio(usidhani nakukebehi, naelewa sana). Sasa kama ilivyokawaida ya Mie, ninapohisi kuwa nimejifunza huwa sio mchoyo ku-share. Hujambo lakini? Unafurahia simu yakoo Mpya(smartphone) ambayo ipo loaded na ma-Apps mwengine wala hujui kazi yake(unadhani yanafanya Simu yako kufanya kazi vema) kumbe katika hali halisi sivyo. Baadhi ya Apps(zile zinazowekwa kila unapo Update Software) huwa zinawekwa na Mitandao husika ili kufuatilia Nyendo zako. Tangu zamani wamekuwa wakifuatilia ili kuboresha Huduma za Mawasiliano, lakini kutokana na uwingi wa Uovu hasa kutoka kwa wenzetu wale Wauaji kwa jina la Dini yao takatifu, hali imekuwa mbaya linapokuja suala la "privacy". Sio Kampuni za Simu tu ndio zinatabia(banwa Kishria) bali pia Facebook, Google na Whassap wanatabia ya kutunza yote unayo-post kwa ajili ya "kuboresha" Huduma zao (wanamaanisha kutunza Data uwekazo kama Ushahidi pale  mambo yamebuna na Serikal

Pale unapokuwa Mke mwema....

....halafu unaonekana sio mwanamke "kamili", kwanini? kwasababu hulalamini-lalamiki pale mumeo anapoacha bafu chafu baada ya kuoga au pengine anachelewa kuamka na kuacha kitanda kipo shagala bagala....(hizi sio kazi za mwanamke ni usafi), huombi-ombi pesa ya manunuzi, Vipodozi wala Salon. Inawezekana upo hivyo kutokana na Malezi/mafunzo uliyopitia au huenda umejifunza kupitia Blogs, maana Siku hizi kuna kila aina ya maelezo yanayotuelekeza namna ya kuwa  Wake(na waume) wema, mengine ni mazuri na mengine yanapotosha.....Akili kumkichwa unapoamua kuchukua na  kujaribu ulichokisoma! Ulalamishi na kutaka jambo/kitu kifanyike pale tunapotaka  ndio  inatufanya wanawake kuwa wanawake (ni sehemu ya uanamke), sasa hayo yakikosekana inakuwa kama vile Mumeo ameoa  mwanaume mwenzie ahahahaha. I mean sawa kujitegemea kiuchumi na kuepuka ulalamishi.....lakini pia tukumbuke kuwa baadhi ya Wanaume hupenda Changamoto Ndoani (sio za kugombana na muumizana mioyo/hisia)! Nat

Urijali/Uanaume Kamili/wa Kweli!

.....hapa lazma nivabe! Lakini kwasababu napenda kuchangia "knowledge" sio mbaya nikikuelezea nilichojifunza. Inawezekana kabisa hukubaliani na ninachotaka kuandika, basi angalau nipe nafasi na unisikilize(soma na share....ahsante). Unajua pale unaanzisha Topic halafu watu wanaivamia na kuaanza Malumbano (ya busara) halafu wewe upo pembeni unafurahia huku  unachukua "Material", basi ndivyo ilivyokuwa. Wengi tunaamini(mie mmoja wao mpaka Wiki Majuzi) kuwa Mwanume Rijal/Kamilii ni yule mwenye Uwezo wa Kusimamisha Uume kwa muda Mrefu au mwenye uwezo wa Kusimama na kufanya mapenzi na kufanikiwa kummimba mwanamke. Baadhi hudhani kuwa Wasenge sio Marijali kwasababu hawapendi wanawake aka hawawezi kuingia ukeni sababu hawawezi kuinuka(Hanithi).....kama Kusimamisha kwa muda mrefu ni Urijali basi hawa  majamaa ni MARIJALI haswa!! Achana na hili. Sehemu ndogo wanaamini kuwa kama Mwanaume  ni Rijali mwanamke mmoja hamtoshi....daah! Ujinga Mzigo. Hawa wan

Knowledge vs Ego....

Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako. Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana. Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!! Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto. Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/K