Za mida hii....? Enzi zile za Usichana(shuleni) kulikuwa na kipindi cha watoto "chuchuchu" kilikuwa kikiendeshwa na Marehemu Amina Chifupa(Pumzika kwa Amani). Alipojifungua basi kila wakati ilikuwa "nani huu hivi, nanihu vile" yaani ali-share excitement ya kuwa mama kwa mara ya kwanza. Mimi na wanafunzi wengine, tulikuwa tunakereka kweli na hiyo "mwanangu hivi, vile".....tukawa tunasema "Amina nae ka' yeye ndio wa kwanza kujifungua, Ulimbukeni tu!! Kumbe bana tulikuwa wadogo, hatukujua hisia anazozipata mwanamke baada ya kujifungua kwa mara ya kwanza. Niulize mimi nilipojifungua mara ya kwanza hehehehehe nilikera watu kwa picha na vijimaandishi vya kuwakilisha vitendo au pose yake kwenye Picha. Hakika niliwakera watu sana tu. Namkumbuka Marco Mwenda (nae ni marehemu alifariki kwa ajari ya Gari mwaka Jana, apumzike kwa Amani)....aliwahi kuniambia " Da' Dinah nawe unachosha, utadhani wewe ndio mama wa kwanza hapa Duniani"......