Skip to main content

1st time Mothers....

Za mida hii....?

Enzi zile za Usichana(shuleni) kulikuwa na kipindi cha watoto "chuchuchu" kilikuwa kikiendeshwa na Marehemu Amina Chifupa(Pumzika kwa Amani).


Alipojifungua basi kila wakati ilikuwa "nani huu hivi, nanihu vile" yaani ali-share excitement ya kuwa mama kwa mara ya kwanza.


Mimi na wanafunzi wengine, tulikuwa tunakereka kweli na hiyo "mwanangu hivi, vile".....tukawa tunasema "Amina nae ka' yeye ndio wa kwanza kujifungua, Ulimbukeni tu!!


Kumbe bana tulikuwa wadogo, hatukujua hisia anazozipata mwanamke baada ya kujifungua kwa mara ya kwanza.


Niulize mimi nilipojifungua mara ya kwanza hehehehehe nilikera watu kwa picha na vijimaandishi vya kuwakilisha vitendo au pose yake kwenye Picha.


Hakika niliwakera watu sana tu. Namkumbuka Marco Mwenda (nae ni marehemu alifariki kwa ajari ya Gari mwaka Jana, apumzike kwa Amani)....aliwahi kuniambia " Da' Dinah nawe unachosha, utadhani wewe ndio mama wa kwanza hapa Duniani"....


.....nikacheka nkamwambia wee ni Mkibaba hujui Mkimama anavyojisikia baada ya kumaliza Miezi Tisa salama na mwishowe kusukuma nje Kilo Tatu za mtu mdogo mwenye afya njema.


Sasa kutokana na Techolojia ilivyokuwa watu wanapitiliza wana-share mpaka Scan ya kwanza(18weeks).....kikwetu hupaswi kusema chochote kuhusu Mimba yako hasa kama haijajitokeza(haionekani) na ukiulizwa unakana...."akuuu sina Mimba mie, Ndoa tu ndio inaninenepeshaa".


Ile hali ya kujifunza na kushuhudia kila hatua ya ukuaji wa mwanao na kuirekodi (asante Teknolojia) ni vere....veri Fascinating.


Kuwa mama sio Kazi rahisi, inachosha inakupa stress na wakati mwingine depression lakini kama una "support system" (ndugu, jamaa na rafiki) nzuri na ya uhakika mambo yanakuwa mazuri sana.


Sasa namuelewa Mama yeyote aliezaa mtoto wake wa kwanza naku-share furaha na yote anayojifunza, shangaa kuhusu mwanae.


Ni hisia maalum ambazo hakuna mwanamke atazielewa mpaka atakapopata uzoefu, na kwa wanaume....well ni wanaume hamtokaa mzijue hisia hizo....hata mkibadilisha Jinsia via Cosmetics Surgery.....hihihihi!

Uanamke ni zaidi ya kupenda mavazi ya Kike, kujiremba, Matiti na Uke....(Nafikiria kwa sauti).

Nikuache kwa sasa eti....babai!
Mapendo tele kwako...
























Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao