Skip to main content

Kila Kidume(secretly) hupenda kidume Maishani....

Hapana sio "Mikorosho" bali kupata/zalishiwa mtoto wa Kiume......Heri ya Wiki Mpya kwako!

Umewahi kutana na wanaume ambao watoto wao wa kwanza ni wa Kike, na ukasikia wanavyotetea Binti zao na kuponda watoto wa kiume au hata kujifanya "hawajali" mtoto gani anazaliwa.


Wengi hudai "Bora Binti Malaya kuliko Kidume Shoga"....ukielewa Sentesi hiyo kwa undani utagundua kuwa Msemaji hapendi watoto wa kike na kesha Muita Malaya kabla hata hajakua masikini.


Hawana mtoto wa Kiume hivyo "ushoga" hausiki (hauna nguvu) hapo lakini tayari wamuita Binti Malaya....haa!


Kisiri-siri wanatamani sana na pengine waliombea kupata mtoto wa kiume lakini haikuwa hivyo.....


Wengine husema "Mheshimu Mkeo kwani kakuzalia kidume muendeleza jina la Ukoo"


Mimi binafsi SIKUTAKA kabisa kuzaa mtoto wa Kike kama 1st born kitambo kabla hata sijajua kama ipo siku nitazaa.


Nadhali ilitokana na hali ya kujisikia "safe" na kuheshimiwa (ogopwa) kwa vile nilikuwa na maKaka.


Nilijiamini kuwa nitatoa Kidume kwasababu kwetu Vidume ni wa kumwaga, pamoja na kujiamini bado haikunipa Guarantee ya mtoto wa kwanza kuwa Kidume.


Hivyo niliomba Mungu kila siku na nilijitahidi kwenye mambo ya "Sayansi ya Viumbe" yaani Tarehe, Mikao na kula aina fulani ya vyakula ili kuongeza "uwezekano" wa kupata Kidume.


Mdogo wangu alipojifungua Mtoto wake wa kwanza wa kiume, nilifurahi huku na natamani/ombea kimoyomoyo ingekuwa mimi.


Zamu yangu ilipofika miaka 2 baadae na Scan ikaonyesha kuwa ni Kidume, nilifurahi hadi nikatoa Sadaka...Team Vidume as 1st Born(doesn't even make sense).


Wa pili sikujali sana (kisiri-siri nilitaka awe mkidada though ili nikamilishe familia).....isingetokea basi ningeasili kabinti mahali.

Siku ya Scan tukaambiwa ni kabinti.....sikufurahi kama ilivyokuwa kwa Kidume lakini nilimwambia baba yake "I told you"(Mimba ilisumbua so nikajua nimebeba mahomono) !!!


Hakika mtoto ni mtoto tu na hatuna budi kushukuru lakini najua sote "kisiri-siri" huwa tuna "prefer" Jinsia fulani, sema guilt, uwoga, au taabu ya kushika mimba/pata mtoto inatufanya tuseme "mie sijali awe wa kike au wa kiume".


Natambua Kiasili na Kisayansi Wanaume wote hupenda kuwa na mtoto wa Kiume. Haina Mfumo Dume na wala sio Chuki ya Gender bali ni hali halisi....ni necha.


Bai kwa sasa...
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi...

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: ...

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao...