Skip to main content

Posts

Showing posts from September 7, 2014

Mwanaume ka' Mwanamke na Nyumba Ndogo!

Only Mwanaume husika akifanya jambo baya, la kizembe au akionyesha "emotions"! Mfano akisema ukweli pasipotakiwa (Umbea), akilia baada ya kuumia, akizimia Msibani (Wanaume hawazimii, huwa wenda wazimu hihihihihi) n.k. Tabia hiyo huwafanya Watoto wa Kiume kuwa na Tabia mbaya za Baba zao, kwasababu wanaogopa au hawataki kufananishwa na Wanawake. Kwenye Jamii yetu (Tz) Baba kuwa na Kimada siku hizi imekuwa suala la kawaida, jamii imelikubali hilo na kuwapa jina zuri eti "Nyumba Ndogo" which is sooooooo annoying, Yaani ndio kukata tamaa au?!! Sasa nyumba ndogo huwa haijengwi kwa siku moja, na mara zote Mtoto wa Kiume huwa wa kwanza kujua ikiwa Baba ana Kimada.....Vijana hujua mengi sana Mtaani/Vijiweni. Wengi huwa wanaumia kuona kuwa Mama zao wanakuwa cheated na Baba zao lakini kwa vile wanaogopa kuitwa "Wanawake" wanaamua Kuuchubua (do you still use this word??). Baadhi ya Vijana (watoto wa kiume) husi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "