Skip to main content

Posts

Showing posts from May 4, 2014

Marehemu....

Mungu aendelee kuwapa Mwanga wa Milele, Amina......hebu ngoja kwanza!! Wameenda wakiwa "wamelala" sasa mwanga wanini wakati wamelala? Ile kasumba ambayo mimi naona ni ubinafsi au kutafuta/taka kuonewa "huruma".....yaani marehebu baba blablabla....Marehemu sijui nani blablabla. Marehemu Baba wa Taifa anatuangalia na kugalauka Kaburini......yaani aache kufanya yaliyomuhimu huko aliko abaki kutuangalia sisi huku na kugalauka kutokana na ujinga au makosa na shida zetu! Sidhani kama hao marehemu huwa hata wanatuombe tulio hai tuendelee kupata "kiza" cha milele ili tusiamke na kukabiliana na shida za Dunia. Mtu akienda, ameenda na huna budi kukubali kuwa kaenda na anaendelea na maisha mengine bila wewe....dizaini ukifa unasahau all bout Dunia na watu wake.....Mambo ya new start...new life. Si wanasema unakuwa "declared dead only" kama Ubonko (Ubongo) haufanyi kazi, sasa kama Ubonko haufanyi kazi kumbukumbu za ya Duniani watazitoa wapi? (In my

Fashenista....

Za jioni? Kabinti kanakua basi sijui ni homono au au kitu gani?!! Khaaaaaaa! Hakajui kuongea basi kila kitu ni "this...this" huku kanasonta (nyooshea kidole) anachokitaka. Unamvalisha Viatu, anaenda kubeba Viatu vingine anataka umvishe juu ya vile ulivyomvisha mwanzo.....Uanamke shughuli, tena kumbe shughuli huanza mapema hivi! Aiiiii.... Ujue...kunatofauti kati ya Kupenda Fashion na Kujua Fashion. Mimi napenda sana tena sana ila sifuati sheria zake(well sizijui na sina muda), navaa ninavyotaka au kujisikia. Sasa kwavile tu napenda Fashion hainipi ruhusa au Mamlaka ya kukuambia uvae nini na wakati gani wakati vaa yangu tu inaashiria nahitaji kuambiwa ninayowaambia wengine. Tangu nimegundua Vlog ayeee nimekuwa addicted, sadly wengi wao ni 20s, which is annoying. Few days ago....oh kiswanhehee....siku chache zilizopita nikakutana na Vloggers ambao wapo 30s aiii nkajiSubie (subscribe). Sasa najifunza kuwa stylist.....natania, una

Kilugha kinakera!

Morning/Noon! Lugha za Tanzania zinaingiliana hivyo hazikeri alafu lazima utaambulia maana kwa mbali hasa kama unatetwa. Kuna Mtangazaji "Tiger beibiiii" wa Ebony ya Iringa huwa ananikosha sana akitumbukizia/nogesha kwa kilugha chake, sio Watangazaji wa Dar wamejaa "you know what I mean" "waraaaap" nyiingi....hiyo sio nukta, nimegusia tu. Lugha za Nchi hii bana ayee! Kichina, Kinigeria, Kipolishi, Kizairwaa, Kisomali, Kirusi na nyingine nyingi....zinakera sana (kwasababu sing'amui kitu). Asa ombea umepanda Basi Moja na Mnaija, Mkongo na Mchina, alafu wapigiwe simu kwa wakati mmoja....Utadhani wamekodisha basi kwa ajili yao tu. Sikuhizi nawaelewa sana Wainglishi wanapoonyesha kukerwa unapoongea Kilugha chako....(Sehemu ni wivu as hawajui lugha nyingine hihihihihi). Huwa siongei Kiswahili ninapokuwa kwenye kadamnasi ya watu ambao najua hawaelewi na kama mazungumzo ni nyeti (lazima kilugha ili wengine was

Daktari na Dawa wanazotupa....

Jambo weye? Umewahi kwenda kwa Daktari ili kuongezewa Dawa unazotumia (repeat prescription) Daktari akakubadilishia Dawa akikuambia "hii ni bora zaidi" kuliko hiyo?!!! Unahofia "side effects" lakini Daktari anakuhakikishia kuwa hakuna baya litakalotokea (niligundua kuwa dawa mpya ni Ghali zaidi kuliko ile ya awali). Jana natazama Documentary (yeah am that boring) nkajifunza kuwa hawa Madaktari tunaowaamini wakati mwingine wanatupa Dawa kama majaribio bila sisi kujua. Na wakati mwingine wanakula Deals na Makapuni ya kutengeneza Dawa ili kufanya Dawa husika kuwa popular au kama sehemu ya Uchunguzi. Ile "kama utapata tatizo lolote tafadhali nipigie simu haraka" hiyo ni report muhimu sana kutoka kwako kuhusu dawa husika. Ushindani wa kuuza Dawa kwenye Makampuni hayo ni mkubwa sana, imefikia mahali Madaktari wana-creat "Disorders" na kula Deals na Wafamasia ili kutengeneza Dawa "kutibu/tuliza Disorders&

Wanyumbani na Wanje....

Heri ya Wiki Mpya! Siku hizi wa Nyumbani na wa Nje zimekuwa "jamii" mbili tofauti wakati zamani tulikuwa kitu kimoja ailimradi tu sote tunatoka Nchi mmoja iitwayo Tanzania. Kuna kama kaushindani au kaubaguzi ka chini kwa chini hivi....well, nilishakuambia kuja Nje siku hizi sio deal labda ndio maana wa nje tunadharauliwa hihihihihi. Alafu tunajifanya tunajua sana utatuzi wa matatizo yanayojiri nyumbani wakati wengine hatujagusa huko mwaka wa Tano huu....kazi kufananisha tu "Kwa mfano huku blablabla" sort of people. Pia kuna wale ambao wapo Nyumbani kazi yao kulinganisha pia....wale akina "when I was in London" kind of people...."Hata wenzetu wa Ulaya blablabla" wakati hujawahi kuishi huko au ulikaa si zaidi ya tumiaka 3. Wote hamna tofauti linapokuja suala la kujifanya mnajua utatuzi wa matatizo yanayojiri Tanzania (hasa kijamii, kisiasa na kiuchumi). Sie wenye watoto wadogo haturudi moja kwa moja