Skip to main content

Marehemu....


Mungu aendelee kuwapa Mwanga wa Milele, Amina......hebu ngoja kwanza!! Wameenda wakiwa "wamelala" sasa mwanga wanini wakati wamelala?



Ile kasumba ambayo mimi naona ni ubinafsi au kutafuta/taka kuonewa "huruma".....yaani marehebu baba blablabla....Marehemu sijui nani blablabla. Marehemu Baba wa Taifa anatuangalia na kugalauka Kaburini......yaani aache kufanya yaliyomuhimu huko aliko abaki kutuangalia sisi huku na kugalauka kutokana na ujinga au makosa na shida zetu!




Sidhani kama hao marehemu huwa hata wanatuombe tulio hai tuendelee kupata "kiza" cha milele ili tusiamke na kukabiliana na shida za Dunia. Mtu akienda, ameenda na huna budi kukubali kuwa kaenda na anaendelea na maisha mengine bila wewe....dizaini ukifa unasahau all bout Dunia na watu wake.....Mambo ya new start...new life.



Si wanasema unakuwa "declared dead only" kama Ubonko (Ubongo) haufanyi kazi, sasa kama Ubonko haufanyi kazi kumbukumbu za ya Duniani watazitoa wapi? (In my head). Usikute Baba yangu kaoa mke mwingine na anawatoto huko wanasoma Shule "international Academia" wakati mie alinipeleka Shule za "Msondo"....nani ataka upweke hapa Duniani....oh kule sio Duniani....aah well!


Muhimu ni kutotaja taja marehemu kila unapokuwa na mashida na mahuzuni yako, "mama angekuwa hai angenishauri"....."Baba ataniongoza tu kwenye hili".....wao hawawataji wana-deal na yao huko waliko. Duh! Baba yangu ni marehemu....hii "Marehemu Baba" haizoeleki....maskini angekuwepo angecheza na wanangu.


Takuona J'3

Kwaheri kwa sasa...
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao