Maoni ya Mhariri...siku hizi sote tunatoa Maoni on particular or similar issues....Teknolojia na Uhuru wa kujieleza/Changia utakacho au ulichokiona/shuhudia unaharibu kazi za watu.
Mfano, kazi ya Uandishi wa Habari wa Magazeti na Radio....imeingiliwa na Blogs, Online Radios, Social Media na YouTube(is YouTube sosho Media pia?).
Jamaa wanatumia Sosho Midia kama "chanzo cha uhakika" na wale Waandishi wavivu wa kukopi na kupesti ndio wamerahisishiwa kazi.
Habari zenye Uzito ni zile za Uchunguzi....labda na mahojiano magumu ya Wanasiasa!
Jana nipo YouTube (napenda Fashion Haul na beauty review....how sad!!?) nikakutana na Matangazo kutoka Kampuni moja kubwa ya Urembo....alietumiwa ni Vlogger na sio Model/Celeb kama nilivyozoea.
Nkajisemea eeh Teknolojia imeharibu na kazi za Celebs na Model pia.....sio haki kabisa!
....Hebu ngoja kwanza! Hawa Vlogger ni real people wanatumia bidhaa na kuzi-review hivyo wao kutangaza bidhaa husika wana...