Tuesday, 7 November 2017

Rudisha Heshima ya Ndoa: Jinsi ya kuepuka Ulalamishi/Kosoaji too Much.


Kama wewe ni Mkosoaji, hii inakuhusu zaidi, Karibu.

Ndoa kama Ndoa ni ngumu na inahitaji  kufanyiwa kazi kila Siku kutoka pande zote mbili. Ndoa  ni ya wawili sio jukumu la Mke tu au Mume tu, bali  nyote kwa pamoja.

-Angalia yaliyo Chanya zaidi ya Hasi.

-Kubali kuwa Makosa yako kimaisha kabla yake(Mwenza wako) hayamuhusu....kwamba kutotimiza Ndoto zako ni Makosa yako wewe na yeye hausiki. Kwa pamoja  manaweza  kukamilisha Ndoto mpya kama Mke na Mume kwa Ushirikiano na Support bila Kumlazimisha afanye yale utakayo wewe kufidia uliyofeli kabla hajakutana.

-Tambua kuwa unaweza kuwa unamjua Mkeo/Mumeo vema sana baada ya kumsoma lakini bado huwezi kamwe kusoma Akili yake. Epuka kusema "najua unachofikiria" "najua unachokitafuta", "najua kwanini unafanya hivyo" n.k....jifunze kutumia maneno "wakati mwingine unanifanya nadhani blah blah blah"...if anything.

-Kubali kuwa wewe haujakamilika, kwasababu mwenza wako hakukosoi au halalamiki haina maana kuwa ana bahati sana kuwa  na wewe "the Perfect one", hata kama aliwahi kukuambia kuwa wewe  ni "perfect" kwake.

-Usifananishe Ndoa ya Fulani na Fulani na kutaka Ndoa yako iwe kama yao. Hujui wanayokabiliana nayo wakifunga Milango ya nyumbani kwao. Ninyi ni watu wanne  tofauti kabisa ambao mmegawanyika katika Mafungu mawili tofauti na kati yenu Wawili bado ni tofauti sio kijinsia tu bali Kimalezi/Mazingira, Kielimu, Kiakili n.k.


Wednesday, 5 July 2017

Rudisha Heshima Ya Ndoa: Mwenza hana Jema, kila siku Kukosoa...Kukosoana ni jambo jema na muhimu ili kusaidia kurekebisha Tabia ndogo-ndogo ambazo ni mbaya lakini kumkosoa  Mwenza wako mara kwa mara (kupitiliza) bila wewe mwenyewe kujali kuwa unakasoro zako ambazo anazivumilia ni wazi utakuwa Mnyanyasaji. Unyanyasaji huo utamfanya mwenzio kujisikia vibaya na hivyo kusababisha:-

-Maumivu ya Hisia na Akili.
-Kumfanya Mwenzio ajione hana thamani au Umuhimu kwenye Ndoa yenu.
-Uoga/Hofu  kwenye Ndoa yenu
-Kuondoa Furaha na hivyo kujitenga kihisia
-Kukosa Amani
-Msongo wa Mawazo


Kwasababu Mwenza wako sio Mlalamishi au Mkosoaji wa mara kwa mara haina maana kuwa wewe ni Mungu na hukosei, kwamba wewe ni next to perfect(hakuna binadamu asie na Kasoro) ndio maana Mkeo/Mumeo hajawahi kukukosoa au kulalamika.


Ukweli ni kuwa, baadhi ya Weza huwa "wanakurekebisha" kwa vitendo, kwamba anafanya exactly vile unapaswa kufanya au kwa kukupa "hints" bila kuumiza Hisia zako wala kusababisha ujisikie vibaya. Asipo pata matokeo ndio anaweza kukuambia.

Ni vigumu sana kuishi na Mwenza wa hivyo kutokana na maumivu anayokupa. Sasa kabla hujaanza kupanga namna ya kuikimbia Ndoa yako, tulia kwanza nikuambie nini cha kufanya, Jinsi ya kuepuka....ila kabla tuanze na sababu zinazoweza kupelekea Mwenza kukukosoa kupita Kiasi(kuku nyanyasa Kihisia/Kiakili).


Nini hasa huwa kinasababisha Mkosoaji kupitiliza?

-Hawana raha/furaha na jinsi walivyo na hivyo wanataka na wewe uwe kama wao bila kujua.

-Majuto; inawezekana kutokana na Makosa yao ya Maisha huko nyuma kabla yako.

-Fainali Uzeeni, hajafanikiwa kukamilisha Ndoto zake na hivyo anatupia "Mpira wa lawama" kwako kama sababu ya yeye kufeli/kutofanikiwa(Wakati hukuwepo wakati wa Ujana wake).

-Malezi/Makuzi  mabovu aliyopitia....ama hakulelewa na Wazazi moja kwa moja  bali Ndugu kama vile Dada/Kaka/Bibi/Babu n.k. kwa zamu,  kwamba hakuwa na "Stable family" utotoni mpaka utu Uzima.


Nini cha kufanya:-

-Usiwe Hasi kwake wala kumkosoa(rudishia). Mwache atiririke na wewe Msikilize kwa makini ili upate materials/points za kutumia Moto wake ukipoa. Usisababishe Mabishano hasa kama mna Watoto.

-Utakuwa umeumia sana kihisia(kwa kawaida kama Mwanamke utakuwa umemchunia), pamoja na maumivu hayo jitahidi kufikiria yote anayokukosoa/lalamikia kila siku. je yanajirudia? je kuna mabadiliko umefanya(jirekebisha)? je haoni jema pamoja na kuwa umejirekebisha? je alikuwa amekunywa kidogo?( ona point ifuatayo hapo chini)

-Baada ya Maumivu/Mnuno/Chunio kuisha, Mwambie ungependa mzungumze. Utakapo anza kuzungumza nae mwambie wazi kuwa ungependa mzungumze na sio mbishane, kwamba akusikilize.

-Ongea nae kwa Upole lakini kwa kumaanisha tena kwa kumuangalia Usoni moja kwa moja. Mwambie tabia yake ya kulalama/kosoa kila akipata nafasi inavyokufana ujisikie. Weka wazi kuwa huna furaha tena kwenye Ndoa yenu kutokana na Tabia yake hiyo mbaya(nafasi yako kumkosoa hii, itumie vizuri. Simamia kwenye yeye kukukosoa kupita kiasi na alivyokufanya ujisikie, mengine save ili usimuumize).

-Mwambie ni sawa kukukosoa lakini sio sahihi kurudia yaleyale kila mara bila kuangalia kama umefanya mabadiliko, pia sio vema kila mnapokuwa pamoja yeye ni kukosoa tu. Mwambie hudhani kuwa hakuna jema hata Dogo ufanyalo na kustahili kukusifia/shukuriwa. Mpe mfano wa Mema unayodhani unafanya kwenye Ndoa  yenu au kwenye Malezi ya Watoto wenu.

-Malizia kwa kusema, nisingependa Ndoa yetu iishie pabaya na nisingependa watoto wetu wawe wanakusikia ukilalamika kila siku kwa mambo yale yale au pengine kusingizia ili upate nafasi ya kukosoa.


Una nyongeza? swali je? tupia humu dinahicious@gmail.com
Sijibu Email moja kwa moja bali nitaweka hapa kwa faida ya wengine.
Nathamini na kujali Muda wako hapa, ahsante.

ooh Post ijayo itakuwa Jisni ya Kuepuka Ukosoaji wa Mara  kwa mara, Usikose
Bai

Tuesday, 4 July 2017

Sababu nyingine kwanini tunawachukia Mawifi....

....(Dada wa Wenza wetu) wa sasa au waliopita(Ex), hasa kama mlizaa kabla hamjakutana au  kabla ya kuachana. Kama uliikosa ile ya mwanzo isome hapa. Hello, ipo jambo?

Madada huwa na viherehere bin vimbelembele vya kutaka kujua kila kitu, hasa Uhusiano ukiwa bado Mpya tangu kuanza/kuisha. wanaweza kujifanya wapo karibu na wewe na wanakupa support, wanakujua na kukupoenda blablabla.


Mawifi hao hao bado ni Shangazi wa Watoto wenu na ni Kaka wa Ex/Current Mumeo,  kwa maana hiyo bado watakuwa karibu na yeyote atakae kuwa na Kaka yao. Hivyo basi kuambiwa/shuhudia mambo mengi/kupewa ripoti kuhusu Mjaza nafasi(mke/Mpenzi mpya) na watoto wake na wakati huohuo wapo karibu na wewe Ex na Watoto wako.


Sasa kama wewe ni Ex au Current one mwenye utimamu hakika utaanza kujiweka  mbali na Mawifi kwa sababu chache zifuatazo:-

-Hawachelewi kukulaumu kuwa umembadilisha Kaka yao.

-Watakuwa wanazungumza na Kaka yao kuhusu Wifi yao wa Sasa na watoto wake na kamwe hawatokuambia(kama wewe ni Ex).

-Watakuwa wanajua kila kitu kuhusu Ex wa Mumeo na watoto wao bila wewe kujua...hasa kama sio muumini wa Blended family(ikiwa wewe ni Current).

-Wanapenda kujimilikisha Watoto wako na kukutenga wewe Mama yao(kama wewe ni Ex).

-Wanaibua Drama bila sababu ya Msingi(wote).

Nini cha kufanya ili kuepuka hayo na mengine uyajuayo:

Pamoja na kuwa Kijamii  Familia Mbili huwa Moja, kwamba mnapofunga Ndoa (au kuwa kwenye Uhusiano wa  muda mrefu) haina maana kuwa hao ni kweli Ndugu zako. Hata siku Moja usijifanye wewe ni Ndugu moja na Ndugu wa Mumeo(kabla hajawa Ex), hata kama wanakupenda kama Peremende.

-Hakikisha Familia yako hajiweki karibu nao
-Waheshimu kama wanavyo kushehimu au kama Dada wa Mumeo, kumbuka Upendo haulazimishwi kama hamja-click  usijipendekeze.

-Kama ni watu wa Drama, wachukulie kama walivyo(a.k.a dharau) na punguza mawasiliano. Kumbuka Wifi hawezi kuwa rafiki hivyo usijiachie sana hata wakiomba radhi.

-Weka mipaka linapokuja suala la Malezi ya watoto wako, ikitokea wameenda  kutembea kwao, wasipofuata matakwa yako, wapige Stop kuchukua wanao(wapwa zao).

-Usiogope kusema Hapana/Sitaki.

Una swali? au Nyongeza?....shoot/share nami dinahicious@gmail.com
Nitaweka hapa kwa faida ya wengine. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai.

Monday, 3 July 2017

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...


...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani?


Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme.


Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme kama uliikosa.


Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe.

-Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa urahisi lakini atakuwa "suprised" na andika "hizi zako, tumia utakavyo", kwa Mfano. Badili ujumbe kila mara unapofanya hivyo.


-Onyesha/toa Shukurani kwa  kazi yake ngumu ya kutoa Malezi mazuri anayowapa watoto, hasa pale unapoona Watoto wanajiamini lakini wana Nidhamu(kuna tofauti kati ya kujiamini na kuwa mtovu wa Nidhamu), kama ni Mama wa Nyumbani. Kumbuka Malezi ni jukumu lenu w ote kama Wazazi lakini kwa Kawaida Mama huchangia zaidi ya Baba, hasa kama Mama huyo ni wa nyumbani.

-Onyesha(onesha) unajali anapokaribia na anapokuwa Hedhini, jifunze namna ya kumpa support, kipindi hiki huwa kigumu kwa baadhi ya Wanawake kama ambavyo ma-teenager huwa japokuwa ni kwa muda mfupi.

-Sifia Mapishi yake na sema Ahsante kila anapokuandalia chakula.

-Usishindane au kulinganisha  "attention" anayotoa Mama kwa  Mtoto/Watoto wenu, wewe ni mtu Mzima unaweza kujihudumia. Watoto bado wanajifunza na wanahitaji "attention" zaidi yako. Mkeo sio Mama yako bali  Mpenzi wako ambae pia ni Mama wa Watoto wenu. Usisahau.

-Mpeleke Manunuzi(Madukani) kila baada ya Muda fulani....sio kwenda kununua Chakula bali mahitaji yake binafsi kama vile Vipodozi, Manukato. Pads n.k,

-Anapokuambia  jambo "serious" hata kama sio hivyo kwako. Msikilize mpaka Mwisho ndio uulize swali, usiulize maswali katikati kabla hajamaliza anachokuambia. au Jitahidi kumsimamisha kwanza alafu ndio uulize....usiulize kwa kuingilia. hii itakusaidi kumuelewa zaidi.

-Jifunze Mzunguuko wake wa Ngono ambao unaenda sambamba na wa Hedhi...zile siku ambazo anakaribia ndio muda Mzuri wa wewe "kulianzisha"....kwa muda wa siku 12 tangu Hedhi kuisha Mkeo hupoteza hali ya kutaka Tendo, sio kwamba hatamani bali anahitaji "msaada" ili kutaka Tendo hivyo ongeza ujuzi kwenye kumuandaa ili kumsaidia kufurahia Tendo atakapokuwa tayari.

-Onyesha au sema adharani kuwa yeye ndio Boss....mf; Dukani, mmenda kununua Kapeti au Gari, pamoja na kuwa Muuzaji anasisitiza ununue na unajua umelipenda lakini Mkeo anaonyesha kusita, mwambie Muuzaji "huyu ndio Boss wangu, Uamuzi wake ni wa Mwisho".

au Mmekutana na "Rafiki" yako ambae hamjakutana kwa  muda mrefu, rafiki anakuomba mkutane Pub, wewe hukupanga kwenda huko siku hiyo, unamrushia Mpira Mkeo..."Mpenzi ulisema baada ya hapa unataka kwenda wapi?".....mkeo atasema atakako hata kama hakuwa na mpango huo, atajua kuwa hutaki kwenda Pub na huyo Mtu.

-Muachie afanye maamuzi kwenye mabadiliko ya Nyumba(ndani), Mambo ya kununua Pazia, Sahani, Sufuria na Mashuka haikuhusu.

-Punguza ukaribu au poteza marafiki wote wa Kike, hata kama ni Dada zako(just saying, females are snakes, I don't even trust myself kama Wifi/Rafiki kwa Wanaume hihihihi).

-Msabahi na Muage kwa Busu na/au Kumbato.....usisahau kumpigia  Simu kumjulia hali unapokuwa mbali na Nyumbani.

-Mueleze(wasiliana) kwa uwazi kuhusu Hofu zako, Shida zako....misukosuko ya Kikazi/Biashara. Hakuna mambo ya "kiume nakabiliana nayo mwenyewe"huyo ni Mkeo ni ubavu wako, mshiriki wako, Mshauri na mtu pekee anaekujua kiundani kuliko hata Wazazi wako...anaweza kukusikiliza na pengine kukusaidia kuondokana na baadhi ya "mambo ya Kiume".

-Usimkosoe/Fokea kabla hujaua sababu ya yeye kufanya alichokifanya au kilichopelekea Mtoto kuumia ambapo wewe unadhani ni Kosa, jifunze kuwasiliana bila kumfanya Mkeo ajisikie vibaya.


Nisikuchoshe si eti?

Una swali? shoot at me on dinahicious@gmail.com. Kumbuka nitakujibu  hapa kwa faida ya wengine wenye swali kama lako na sio kwa Email. Shukurani kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa nathamini na kujali Muda wako hapa.


Bai.

Thursday, 6 April 2017

Wenye Ndoa, tuache kuwabadilisha Waume Zetu.Sasa kabla hatujaanza kumsimamnga Wifi kambadilisha Kaka yetu, tuangalie kwanza Wifi alikuwa nani kwao, na je uamuzi wa Wifi kupumzika ki-career baada ya Kuzaa ni kum-support Kaka yenu(Mumewe) ki-career au ni njia tu ya yeye kula Mahela ya Kaka yenu? Je ndugu zake waliokuwa wakimtegemea hawateseki kwa kukosa "kipato" kutoka kwa Dada/Mwana wao?Kwenye era hii ya Sosho Midia inabidi uwe makini sana maana info ni za kumwaga(tofauti na 2007 nilipoanza  kublog), ni kweli baadhi zinasaidia hasa zile za Medical kutoka kwenye Site za Shirika la Ugojwa husika au Shirika la Afya Duniani. Lakini linapokuja suala la Ndoa au mahusiano, ongeza umakini kwasababu Ndoa hazina Kanuni Moja na watu hatufanani hata kama tulikaa tumbo Moja Miezi 9 na kuzaliwa kupitia Njia mooja na siku Moja bado tutatofautiana kwa kiasi fulani.Maisha magumu, kila mtu anatafuta views na clicks siku hizi, mara zote(kama Wanasiasa) watu huamua kuongea au kuandika mambo ambayo wanajua watu watakuja mbio kutaka kuona/jua. Labda ni kwavile ndio wanachopitia hivi sasa au wanajiandaa just incase ikitokea watakuwa wanajua namna ya kupambana.Siku moja "nilitumiwa" Video ya Mwanamke(as you do) akiwaasa  Wanawake kama yeye kutowabadilisha Waume zao na kukamata Pesa zao na hivyo Waume hao "kusahau" Familia zao. Nikaendelea kusikiliza nikiamini kuwa anawazungumzia Vimada in which nilianza kumuunga Mkono.


Baadae akasema "utakuta Umeolewa na Mwanaume ambae alikuwa anategemewa na familia yake, lakini baada ya muda unambadilisha Mumeo na kuitelekeza Familia yake. Familia  yake inateseka kwa ajili yako. Familia uliyomkuta nayo, iliyomlea, tuache kuwabadili Waume zetu". mmmh!


Nikajisemea "huyu Dada lazma hajasoma (hana Elimu ya juu) au ameolewa akiwa hana Kazi wala Majukumu kwenye Familia  yake(Wazazi na Ndugu zake). Kuna akina sie ambao tulikuwa tunategemewa pia na Familia zetu, mpaka baada ya Kuzaa na Waume zetu. Je kuna mtu anaenda kueneza "Neno" kuwa Waume zetu wasitubadilishe Wake zao?Wazazi wetu (sisi Wake) hawakutumia Pesa zao kutusomesha na kutupa maadili mema ili tuje "kuzalishwa" a.k.a "haribiwa shape" na kuacha Career zetu kwa Muda ili tulee watoto ambao wanabeba Jina lenu la Ukoo. Hebu wekeni Heshima, ebo!Sijawahi kusikia mtu yeyote akilalamika kuwa Wake tumebadilishwa na Waume zetu baada ya kufunga nao ndoa, sio kwamba "hawatubadilishi" la hasha! tunabadilishwa pia.....tena sio kubadilishwa hehehehe, tunaharibiwa Shape na isitoshe kupatwa na Maradhi ya ajabu ajabu for the rest of our lives.Sidhani kuwa tunawabadilisha Waume zetu, bali Majukumu na Vipaumbele vinabadilika. Watoto na Mkewe wanakuwa muhimu zaidi kwake kuliko Ndugu zake. Ndugu zake wamekua/watakuwa na maisha yao bila yeye. Yeye hakuwaleta Ndugu zake Duniani bali Wazazi wenu, kama yeye alivyo Mzazi kwa Watoto wake.Kuna wakati Maisha hubadilika(mtu unakua mtu Mzima), Familia yako inakuwa Wewe, Mkeo/Mumeo na Watoto wenu. Wale mliozaliwa pamoja kama Familia mnakuwa sio "Familia" tena, mnabaki kuwa Ndugu wa Damu. Upendo na uzito/umuhimu upo  pale pale, mtasaidiana ktk shida na mtatembeleana lakini hauwezi kuwa Tegemeo lao Kiuchumi.Sawa, huyo ni Kaka yenu ambae ni Mume wa Mtu mwingine(Wifi yenu), mnamjua Kaka yenu tangu utoto wake lakini Mkewe anamjua Kaka yenu  katika Kiwango kingine tofauti na cha kipekee ambacho hata mfanye nini hamuwezi kumjua kihivyo(sizungumzii Ngono hapa), sio nyie tu  Ndugu zake bali hata Baba na Mama yenu.


Nathamini muda wako hapa, shukrani kwa kunichagua Mie leo.
Noo see ye efter.

Wednesday, 5 April 2017

Akisema "tafuta mwingine, mie siwezi/nimechoka"....


...hamaanishi kwamba ukatafute  kweli mwingine, anachomaanisha ni kuwa "nibembeleze na unihakikishie kuwa utanivumilia" mpaka nitakapo kaa sawa Kihomono au kupona(kama alikuwa anaumwa)....Za Miezi Miwili/Mitatu? hello, jambo jambo!!


Kwa kawaida Mume anapopatwa na tatizo kubwa litakalomfanya ashindwe kutekeleza Majukumu yake kama Baba na Mume, Mwanamke atavumilia na kumuuguza, kumpa Moyo na Matumaini. Lakini Mwanamke akijifungua(zaa) achilia mbali kuugua....katoa Uhai wa Mtu salama baada ya Miezi 9 kukaa na kulala kwa tabu.


Mara zote kipindi hiki huwa Kigumu sana japokuwa kasumba ya Jamii "kukuharakisha" upone haraka huficha ukweli kuwa Mwanamke anapojifungua hukabiliana na mambo mengi Kiafya(kimwili, kihisia na kiakili). Hali ambayo hufanya baadhi ya Wanaume kuamini kuwa Mimba na kuzaa ni "cha mtoto" tu, sio kazi(kama alivyo pizi ndani ya dakika zake 3 kwa utambu uliodumu kwa sekunde 90)....hakuna ugumu wowote, fyatueni tu.Kwa kawaida(uzoefu wangu) Mwanamke anapona pale alipotokea Mtoto ndani ya Wiki 4, lakini wapo baadhi huendelea "kuumwa" mpaka Miezi 3 au Sita. Kipindi hiki huesabiwa kuwa ni kigumu kwa Mume, kwasababu atapata wapi Tendo la Ndoa ikiwa Mkewe bado "anaumwa" kwa muda mrefu hivyo.Presha hii siku zote hutoka kwa Wanawake wenzetu huko nje, na ndani huwa Mume husika(hasa kama sio muelevu). Mumeo anaweza kulalamika kwasababu haelewi unachokabiliana nacho na hivyo mnaweza kugombana(zozana) kutokana na upungufu au "uchelewaji" wa kurudia hali yako ya kawaida.


Kwa hasira hapo mwanamke anaweza kusema kama unashindwa kuvumilia mpaka nitakapo pona basi nenda katafute Mtu mwingine, mie siwezi! Mara nyingi hapa Mwanaume wa kipuuzi atakaa kimya akijua kapewa ruhusa.


Lakini Mume mwema na mwelevu atajitahidi kujua kwa undani kinachomsumbua mkewe, ataomba radhi na kuahidi kuendelea kuvumilia. Atakuwa karibu na Mkewe na kutoa ushirikiano zaidi. Wakati mwingine ushirikiano na uelevu wa  masuala ya uzazi kwa Mwanamke husaidia kwa kiasi kikubwa uponaji wa Mkeo baada ya kujifungua.


Sasa anaposema, "tafuta mwingine, mie siwezi" humaanisha "nipe ushirikiano, nielewe, nivumilie na unihakikishie kuwa huendi popote mpaka akae sawa".

Yep! Wanawake (karibu wote) hata mie ambae ni straight foward no corner kuna wakati namaanisha kitu kingine kabisa tofauti  na ninachomwambia Asali wa Moyo.....hasa nikiwa na Hasira.Pamoja na kusema hayo yoooote hapo juu bado kama Mke  unaweza kutumia Kazi ya Mikono, Mdomo, Mipaka ya Makalio au vilevile unaweza kuongeza ukaribu na Mumeo kwa namna nyingine. Ila kuwa makini kwasababu Nyege zikikupanda ni wazi utapata "maumivu" fulani hivi maeneo ya K, nje na ndani kutokana na Msukumo wa Damu....bila Msukumo wa Damu, hakuna Nyege. eeeeh Moyo Sukuma Damu na si vingine, hihihihihi Ditto knew that akakupotosha!!Endelea kuwepo, Post ijayo tuangalie jinsi Mke anavyolaumiwa "kumbadili" Mume asiipende na kujali Ndugu zake kwenye Ndoa. Je ni kweli tunawabadili? vipi kuhusu sisi Wake ambao  labda tulikuwa tunategemewa na Ndugu zetu lakini tukaacha "Career" zetu na kuwazalia/kuwalelea watoto wao? Usikuse.

Shukrani kwa Ushirikiano.

Babai.

Monday, 23 January 2017

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mumeo ajihisi "Mfalme"....

Waliposema "ajihisi Mfalme" hawakumanisha akutawale na kukutumikisha wewe Mkewe kama Mtumwa wake na hivyo kukosa sauti na kubaki "Ndio bwana", bali kufurahia maisha ya Ndoa na hivyo kurudisha ufanyao ili na wewe ujihisi "Malkia"......Heri ya Mwaka mpya 2017!!


Mie kama Mwanandoa wa "Kitambo" sasa nimeamua Mwaka huu kurudisha Heshima ya Ndoa baada ya kuona kuwa watu wanapotosha na  hivyo Ndoa kuonekana kuwa ni Kazi...well ni Kazi ya pili baada ya ile uifanyayo kukupatia Kipato au ya Tatu ikiwa mna watoto, lakini sio Kazi kwamba ni ngumu na ukibaki humo basi wewe ni Shujaa. Hapana!


Upotoshaji huo unapelekea baadhi ya watu waliokwisha "onja" Ndoa na baadae kuharibika kuchekwa/shangawa kwanini wanarudi tena Ndoani(na watu mwingine) wakati tayari wanajua "maumivu" ya Ndoa....Vijana wamekuwa wakiiogopa Ndoa.


Kwasababu Ndoa moja imeharibika haina maana zote zitakuwa kama hiyo iliyopita. kumbuka watu wanatofautiana na pia kuna baadhi wanaamini katika Mapenzi na Ndoa, wanapenda kuwa kwenye Ndoa na hivyo hawaogopi kujaribu tena na kufanya mabadiliko.


Ndoa ni mtindo wa Maisha mzuri sana tu, hasa ikiwa wote wawili mlijiandaa kuungana kuwa kitu kimoja, mpo tayari kujifunza, kushirikiana, kuwajibika(fanyia kazi Ndoa yenu) na Makubaliano yenu hayo yaliegemea zaidi Upendo na Urafiki....sio Elimu, Pesa au Mafanikio yenu au  Familia zenu(inasaidia lakini sio lazima).


Wengi huamini kuwa Wanaume ni wagumu sana kuridhishwa lakini kwa Uzoefu wangu uliochanganyika na "common sense" Wanaume are very simple ukiwajulia. Aachana na hili, twende kwenye ku-Mflame-nisha Mumeo sasa.Kwa kawaida kila Mwanaume(Mume) huwa  na yake apendayo  kufanyiwa na hivyo kujihisi ni "Mfalme" kwasababu Binadamu tunatofautiana, lakini pia kuna yale mambo ambayo ni ya kiujumla. Kwamba haijalishi ni aina gani ya Mwanaume...ukimfanyia yafuatayo(kama hujawahi kuyafanya) hakika utamfanya awahi kurudi Nyumbani kila siku na kutaka kuacha Kazi zake ili abaki nawe nyumbani(halafu sijui mtakula nini?):-


-Muweke Mungu wenu karibu(inategemea na Imani zenu), Ombeni pamoja na umuombee yeye zaidi  kuliko kujiombea wewe mwenyewe.


-Onyesha unajali, thamini, shukuru na kutambua Juhudi zake kwenye shughuli zake za kila siku za kuwaingizia Kipato. Mfanye awe Shujaa wako hata kama unaingiza Pesa nyingi zaidi yake au zaidi ya Baba yako.


-Akitoka, mcheck kujua kama yupo Salama, kwa kawaida utakuwa unajua kaenda wapi (lazima atakuambia)na atakuwa huko kwa Muda gani (+ Usafiri). Mfano kwenda na kurudi ni Dakika 40 nzima, akakuambia atakuwa Pub mpaka Mpira Uishe then usim-check mpaka Mpira uishe. again kwa kawaida atakujulisha kuwa sasa anatoka Pub n.k.


-Lianzishe angalau mara 3 kwa Wiki(inategemea mnafanya mara ngapi kwa Wiki, lianzishe mara nyingi zaidi kuliko yeye), Hapana Mumeo hawazi  kuhusu kufanya mapenzi muda wote na pengine anaweza kukuambia kuwa "kufanya mapenzi sio lazima" lakini ni Muhimu...hapo anamaanisha kuna siku/wakati hajisikii laikini ukimuonyesha njia basi atakufuata  na atamaliza safari na wewe(kama sio kabla yako).-Tengeneza Mazingira ya Amani hapo Nyumbani, kwa maana ya kujifunza kudhibiti au Punguza Kisirani(zijue Tarehe zako  na utafute mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya Homono unapokaribia Hedhi na pengine Wakati wa Hedhi), sio rahisi lakini inawezekana.


-Amka nae Asubuhi na umuandalie Kifungua kinywa au kama Usingizi wako ni Muhimu zaidi(kama mimi) basi muandalie Chakula cha Mchana ambacho atakula akiwa Kazini. Kwa wale ambao labda hili ni gumu  kutokana na Mazingira au Hali ya Hewa basi Muandalie Nguo za kuvaa kabla ya Siku husika.


-Toa Mkando, Mkande Mumeo mara baada ya kushusha "mabegi" yake ya Kazini(kama unapokea, basi pokea, mie huwa sipokei), mjulie hali huku unamkanda maeneo ya Mabegani na mgongoni, najua kama mna watoto watakuja na kutaka kufanya ufanyavyo kwa Baba yao. Usiwafukuze, waache wajifunze.

-Onyesha kuwa unampenda bila kumwambia unampenda, unaweza kutumia Busu, Kumkumbatia kwa namna ambayo inasema nahitaji uwepo wako, kumpikia vizuri, jinsi unavyo mtazama n.k


-Achana na Mambo ya Zamu yako kuosha vyombo sijui kupika au kuogesha Watoto n.k na badala yake anza kufanya kitu halafu muombe aje/aende kukusaidia kufanya jambo lingine. Jifunze kuzungumza/Wasiliana zaidi kuliko kulalamika.


-Anapokuwa  na Watoto usimuingilie, kumbuka kuna aina ya Kimalezi mnafanya pamoja kama Wazazi (Timu) lakini pia kuna baadhi huwa unafanya kama Mama, sasa muache na yeye afanye kama Baba. Kila Mzazi anasehemu yake maalum na ya kipekee kwenye maisha ya Mtoto/Watoto.-Jitahidi kufanya Tendo kila Asubuhi, hii ni tofauti na namba 3 ya "Kulianzisha"...hii haihesabiki kwasababu huwa Kasimama tu na sio kwamba anataka Tendo, lakini ukimgusa/kumbatia lazma ata-respond kivingine au wewe mwenyewe Ukiguswa na kitu kigumu asubuhi utatamani iingie mahala. Halafu sababu nyingine inayofanya "cha asubuhi" kisihesabike ni kwamba wewe na yeye actully mna kuwa sleepy and lazy hihihihihi. Hii ni Salamu tu.


-Usafi wa Nyumba(Mazingira), na wewe mwenyewe kujipenda/pendeza.


Nikutakie siku Njema, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai bai.